Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe; BOSCO MWANGIDE amesema Serikali haitavumilia kuona uharibifu wa mazingira kwa sababu yoyote ile unaendelea kufanyika wilayani Chunya, Hivyo kila atakaye bainika kuharibu mazingira sheria, kanuni na taratibu zitazingatiwa ili kumuwajibisha mtu huyo
Mwanginde alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kitongoji cha Idendeluka kilichopo kijiji cha Sangambi kata ya Sangambi na kueleza msimamo wa serikali kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa kupitia Uchomaji wa Mkaa katika kitongoji hicho.
“Wako watu ambao si waaminifu na wanaona miti hii kama ni zawadi yao peke yao, wanaanza kuifanyia fujo, wanaikata na kuwanufaisha wao peke yao kitu ambacho mimi kama mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Sitakubali kabisa kwani Mimi nipewa dhamana ya kusimamia shughuli za maendeleo Chunya hivyo katika kipindi change Mimi nitapambana nao sana hawa wanaoharibu Mazingira kwa manufaa yao”
Awali akitoa salamu kwa wananchi Diwani wa kata ya Chalangwa Mhe Haji Chapa amesema Mazingira hayana mipaka hivyo yeye kufika katika kata ya Sangambi ni kutambua umuhimu wa mazingira na hatimaye kushirikiana pamoja kuhakikisha mazingira yanatunzwa
“Uharibifu wa mazingira hauna mipaka kwani ukame hautasema miti imekatwa sana Idendeluka basi ukame utakuwa idendeluka, ukame utakuwa kote wilaya ya Chunya kwa ujumla, hivyo tumefika hapa ili tuweze kupambana kwa pamoja kuhakikisha tunalinda mazingira pamoja na uharibifu unaofanywa katika maeneo haya ni mkubwa sana”
Diwani mwenyeji wa Kata ya Sangambi Mhe JUNJULU NDETE amesema haiwezekani viongozi wetu wa kitaifa wanahangaika kupambana kuhakikisha mazingira yanalindwa lakini sisi tunaharibu mazingira bila utaratibu hilo halitavumiliwa kabisa
“Vyomba vya habari vinaeleza namna ambavyo makamu wa Rais Mhe Dkt Philip Mpango ameonekana maeneo mbalimbali akizindua program za kupanda miti maeneo mbalimbali je sisi ni akina nani tukate miti bila kupanda miti? Hili mimi sitavumila kabisa”
Innocent Lupembe afisa misitu Mkuu (TFS) wilaya ya Chunya amesema wilaya ya Chunya hasa katika kitongoji cha Idendeluka ina uharibifu mkubwa wa mazingira na ndio sababu kubwa iliyopelekea uwepo wa mkutano huo ili kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ukizingatia eneo hilo mbali ya kuwa moja ya Chanzo cha Maji kuelekea bonde la usangu na hata maji kwaajili ya matumizi ya wananchi wanaoishi katika maeneo hayo
Mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na uharibifu wa Mazingira hasa ukataji wa miti kwa ajili ya uchomaji mkaa na kilimo jambo ambalo linahitaji nguvu za pamoja kuhakikisha uharibifu huo unakomeshwa ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza hapo Mbeleni ikiwepo ukame, njaa na hata mafuriko.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ataendelea na ziara hiyo ya kutoa elimu kuhusu Utunzaji wa mazingira na kueleza msimamo wa serikali juu ya utunzaji wa mazingira tena leo 5/4/2023 katika kijiji cha Shoga ambapo mkutano wa hadhara utafanyika katika Kitongoji cha Tukuyu, Lengo likiwa ni kuhakikisha mazingira yanakuwa salama kwa ustawi wa viumbe hai na jamii kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo yao kwani ajenda ya ukusanyaji wa mapato wilayani Chunya ni agenda ya Kudumu
Mhe. Mwanginde ametoa kauli hiyo mapema leo wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Chunya kilichoketi leo tarehe 3/3/2023 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) ambapo taarifa mbalimbali kutoka kamati mbalimbali zimejadiliwa
“Twende tukasimamie miradi lakini twende tukasimamie, mapato ukusanyaji wa mapato ni ajenda ya kudumu ya baraza lolote lile hasa likiwemo baraza la halmashauri ya wilaya ya Chunya” amesema Mhe. Mwanginde
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Simon Mayeka alikuwa sehemu ya kikao hicho amesema wilaya ya Chunya kwa mujibu wa Ongezeko la watu kwa asilimia mia moja na ishirini (120) kwa sense ya watu na makazi ya Mwaka 2022 ukilinganisha na idadi ya watu kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012
“Chunya sasa ina jumla ya watu laki tatu arobaini na nne elfu, mia nne sabini na moja 344,471 ambayo ni ongezeko la karibu asilimia mia moja na ishirini (120) kutoka Laki moja hamsini na sita elfu na mia saba themanini na sita (156,786) kwa sense ya mwaka 2012, Katika idadi hiyo wanaume ni 176,457 sawa na asilimia 51 huku wanawake wakiwa ni 168014 sawa na 49%”
Mhe. Mayeka ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia na kufanikisha zoezi la sense ambapo Chunya sasa kupitia matokeo ya sensa tunaweza kujua namna sahihi ya kupanga mipango ya kiuchumi na maendeleo kwa ujumla
“Mweshimiwa Mwenyekiti naomba kuzishukuru serikali zote mbili kwa kusimamia kwa mafanikio makubwa na hatimaye sasa tunayo matokeo ya sense kwa ngazi za wilaya, kata na nimeambiwa kwamba tutapata pia sense ya watu na makazi kwa ngazi ya vijiji kadiri uchakataji unavyoendela”
Aidha Mkuu wa wilaya ya Chunya amekemea vikali mawakala wa fedha kuchaji fedha ya ziada kwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo amesema ni kinyume na Sheria hivyo amemuagiza Mkuu wa polisi wilayani Humo kuanza kuwakamata wale wote watakaobainika kufanya hivyo.
“OCD kuanzia leo polisi kata popote walipo waanze kuwakamata mawakala wote wanaowatoza fedha wananchi wanapohitaji huduma ya kutuma fedha jambo ambalo ni kinyume na utaratibu hivyo kuanzia leo polisi kata wapewe maelekezo ya kutekeleza agizo hilo”
Mkuu wa wilaya ya Chyuna ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa madiwani kwamba kuna mawakala wa fedha wanamtaka mwananchi kutoa shilingi miatano ili awekewe shilingi Elfu kumi (10,000/=) hivyo kumfanya mwananchi atoe elfu kumi na mia tano wakati pesa atakayowekewa kwenye simu yake ni shilingi elfu kumi (10,000/=)
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya Ndugu Noel Chiwanga amewapongeza waheshimiwa Madiwani namna wanavyotekeleza majuku yao hasa usimamizi wa fedha za miradi mbalimbali zinazotolewa na serikali ya Jamhuri ya Munngano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
Pia amepongeza serikali kwa ujumla, kamati ya ulinzi na usalama na Baraza la Madiwani namna walivyosimamia suala la wanafunzi kuripoti shule kwani serikali imejenga madarasa ya kutosha hivyo lazima wanafunzi wakasome, hivyo mmefanya kazi kubwa na nzuri kuhakikisha watoto wetu wanenda shule
“Mkurugenzi wetu unafanya kazi nzuri kwenye usimamizi wa miradi, tumepita huko nje na tumeona, Hongera sana Mkurugenzi, Lakini kuna baadhi ya wakuu wako wa idara hawakutendei haki na tumejipanga siku moja tutakuja tuongee na wakuu wa idara pamoja na watumishi wengine ili kujenga umoja sahihi maana sisi Chama na Serikali ni kitu kimoja”
Kikao hiki cha Baraza la Madiwani ni kikao cha Kawaida cha Baraza hilo, ikiwa ni kikao cha Robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kupitia vikao kama hivyo wilaya ya Chunya imeendelea kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya ambapo Mpaka sasa inaongoza kwa ukusanyaji wa Mapato katika Mkoa, imeongoza katika suala la Lishe na maeneo mengine mengi
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.