HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA
IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
a) Idadi ya Mifugo
Ufugaji wa wanyama ni miongoni mwa shughuli muhimu za kiuchumi kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya. Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inakadiliwa kuwa na mifugo 4,229,964 ambapo kati ya hao Ng’ombe ni 327,547, Mbuzi 34,447 ,Kondoo 14,627,Wanyama wengine wanaofugwa ni pamoja na Punda 1787,kuku 143,861, Nguruwe, 2695 na mbwa 5,214.
b) Miundombinu ya Mifugo/Uvuvi
Wilaya ina jumla ya Miundombinu ya Mifugo na Uvuvi kama ifuatavyo Majosho Kumi na mawili (120) ambapo kati ya hayo 8 yanamilikiwa na Serikali na 4 yanamilikiwa na watu/vikundi vya wafugaji, Malambo ya maji manne (4),Vibanio vya chanjo viwili(2),Pepea(Windmill) tatu (3), Machinjio ndogo( Slaughter slabs) tatu zilizopo Chunya mjini kata ya Itewe,Makongolosi na kata ya Lupa Tingatinga.
Pia Halmashauri ina jumla ya minada ya mifugo saba (7), mabwawa ya samaki tisa (9)
c) Eneo la Malisho
Wilaya ina jumla ya eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho lenye ukubwa wa 1,050,950.2, na kati ya hilo eneo Lililopimwa ni 533,938.92 na,Lililohuishwa 74499.62, Halmashauri ina jumla ya vijiji 43 na kati ya hivyo Vijiji vilivyofanyiwa matumizi bora ya ardhi ni vijiji 14.
d) Wataalamu wa Mifugo/Uvuvi
Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya wataalamu wa Mifugo Kumi na mmoja (11) ambapo kati ya hao watatu (3) wapo makao makuu na wanane (8) wapo katika ngazi ya kata. Lakini pia Halmashauri haina mtaalamu wa Uvuvi.
e) Vyama vya Ushirika
Halmashauri ina jumla ya vyama vya ushirika Kimoja (1) kinachoitwa Hiyari ya Moyo kinachopatikana katika Kata ya Sangambi na kijiji cha Shoga chenye wanachama 54. Chama kinajihusisha na ufugaji wa Ng’ombe wa nyama.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.