Wadau wa michezo Wilayani Chunya wameungana na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapa vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na madaftari , kalamu , mashati ya shule , mchele, mafuta , sabuni na mahitaji mengine ambayo yatawasaidia wanafunzi hao kukidhi mahitaji yao.
Wadau hao wa michezo kutoka Mbeya motor sport club, Ngindo campany limited, Mapesa company limited na Nyondo company limited wametoa vifaa vya hivyo pamoja na chakula leo tarehe 13/02/2026 katika Shule za msingi sita (6) zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Mkuu wa kitengo cha utamaduni Sanaa na michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Coretha Kalanje pamoja na kuwashukuru wadau hao wamichezo kwa misada mbalimbali waliyoitoa kwa wanafunzi wenye mahitaji ,pia ametoa rai kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza katika kuendeleza sekta ya michezo ili kudumisha umoja, ushirikiano na utamaduni kwa usatawi wa jamii katika nyanja za kiuchumi na burudani
Afisa elim Maalum Wilaya ya Chunya Bi Hawa Mtonyole amesema kuwa jumla ya wanafunzi 252 wamenufaika na misaada ya wadau hao huku akiwaomba wadau wengine kuendelee kujitokeza na kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye mazingira magumu na wenye mahitaji maalum kwani bado watoto hao wanauhitaji mkubwa.
“Tunawashukuru sana wadau kwa kuwaona watoto hawa wenye mahitaji kwa kuwapa madaftari na vifaa vingine kwani vitawasaidia katika masomo yao ikiwa ni pamoja na kuandika , pia tunawashukuru wadau kwa kutuletea chakula kwa watoto wenye mahitaji maalum hapa Shule ya msingi kibaoni kwani wanauhitaji mkubwa wa chakula lakini pia bado tuna wanafunzi wengine wenye mahitaji maalum katika kituo cha lupa tingatinga na Makongolosi” Amesema Mwl Mtonyole
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wadauhao wa michezo ndugu Steven Nyondo , ndugu Alex Mpoma , Wesday Nyondo, Joyce Ndolela wamesema kuwa mbali na kuwa wameandaa mashindano ya mchezo wa magari (drift) lakini pia wao kwa umoja wao wameona nivema kuwatembelea na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitahi maalum na wanaoishi kwenye mazngira magum ili kuweza kuwasaidia mahitaji yao .
Mwalim Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Mbugani Mwalim Jocia Ndalo amesema kuwa vifaa walivyopoewa wanafunzi wenye mahitaji maalum na wanaoishi mazingira magumu vitawasaidia kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili ikiwa ni pamoja na kushindwa kuandika kwasababu yakukosa madaftari pamoja na adha nyingine.
Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wengine bi Sheila Amon na Ndugu Ezekiel Elias wamewashukuru wadau wa michezo kwa misada mbalimbali waliyoitoa ikiwa ni pamoja na madaftari kalam, soksi masharti ,chakula na vifaa vingine huku wakiahdi kusoma kwa bidi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mchezo wa magari( drif ) ulioandaliwa na wadau wa michezo unaotarajia kufanyika tarehe 14/02/2026 ambapo leo tarehe 13/02/2026 wadau hao wamewatembelea wanafunzi wenye mahitaji maalum na wanaoishi mazingira magum na kuwapa vifaa mbalimbali vya Shule pamoja na chakula katika shule sita (6) za msingi ikiwa ni pamoja na Shule ya msngi Chokaa, Kibaoni, Kiwanja, Mbugani Chunya Mjini na Chunya kati .

Mwenyekiti wa Mbeya Motor sport club Ndugu Steven Nyondo akikabidhi madaftari na kalam bi Sheila Amoni mmoja ya wanufaika wa msaada huo kkatika Shule ya msingi Chokaa.

Baadhi ya misaada iliyokabidhiwa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum Shule ya msingi kibaoni ikiwa ni pamoja na Sabuni, Mchele , mafuta ya kupikia, madaftari, na vitu vingine .

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mgugani wakiwa wameshika madaftari, kalamu ,rula na penseli vifaa ambavyo wamekabidhiwa na wadau wa michezo ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.