Mkuu wa idara ya elimu ya awali na Msingi Mw Marko I. Busungu amewataka walimu waliopewa vifaa visaidizi katika kutekeleza majukumu yao kuhakikisha wanavitunza vizuri ili viweze kuwasaidia kwa muda mrefu kwakufanya hivyo watakuwa wamemtendea haki Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani yeye ndiye aliyewapatia vifaa hivyo.
Ametoa rai hiyo mapema leo 27.01.2026 ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo kwa wahusika ili viweze kuanza kufanya kazi kama Serikali ilivyoelekeza.
“Naomba nitoe rai kwa walengwa wa vifaa hivi, wakatunze vizuri ili viweze kutumika kwa muda mrefu zaidi na kwakufanya hivyo mtakuwa mmemtendea haki Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani yeye ndiye aliyetoa vifaa hivyo kwaajili ya matumizi yenu kuwarahisisha mkiwa mnatekeleza majukumu yenu ya kila siku” Amesema Mw Busungu
Aidha Mw Busungu ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kipindi cha pili kuwakumbuka walimu wenye mahitaji maalum kwani nao ni watumishi kama watumishi wengine hivyo kuwapatia vifaa kutawapa uhuru wa kufanya kazi lakini pia watajiona nao kuwa sehemu ya jamii wanayoitumikia
Naye Afisa Elimu Maalum Bi Hawa Mtonyole amesema Halmashauri ya wilaya ya Chunya ina walimu wanne wenye mahitaji maalumu, wawili kati ya hao wamepatiwa vifaa visaidizi kama vile Kishikwambi Pamoja na Kompyuta Mpakato huku walimu wengine wakiendelea kusubiri vifaa hivyo kulingana na uhitaji walio nao.
“Chunya tuna walimu wanne wenye mahitaji maalumu. Mwalim Mwatimba yeye amepatiwa Kishikwambi, Mwalimu wa Bitimanya sekondari amepewa Kompyuta Mpakato wakati mwalim wetu wa Shule ya Sekondari Itewe atapatiwa Kitimwendo kwaajili ya kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake, pia Mwalim mwingine mwenye ulemavu Ngozi naye atapatiwa. Mhe Rais amesema walimu wote wenye mahitaji maalum watafikiwa ili kurahisisha utekelezaji wa Majuku yao” Amesema Mw Mtonyole
Mwalim Edward Mwatimba ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum na hatimaye kuwapatia vifaa visaidizi ambavyo vitasaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku
Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndani ya siku 100 za Mhe Rais imepokea fedha, imepokea watumishi ajira mpya Pamoja na mambo mbalimbali na sasa watumishi walimu wenye mahitaji maalum wamefikiwa kwakupatiwa vifaa visaidizi.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ili kujua mambo mengine mengi
Youtube: Chunyadc Online
Facebook: Chunya Dc na Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Instagram: Chunyadc_official

Baadhi ya vifaa visaidizi walivyopatiwa walimu wenye mahitaji maalumu

Mw Hawa Mtionyole Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati akifafanua jambo wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa visaidizi kwa walimu wenye mahitaji maalum

Mw Abibu Edward Mwatimba wa Shule ya Msingi Kibaoni akitoa shukrani zake kwa niaba ya walimu wengine (Mkononi ameshika Kishikwambi) baada ya kukabidhiwa kifaa saidizi kwaajili ya matumizi yake
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.