Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa Pamoja wamewataka wananchi wa Chunya kuendelea kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao kwani Mafunzo waliyoyapata katika semina elekezi yamepata mwanga wa namna sahihi ya kuwatumikia wananchi waliowaamini na kuwachagua kuongoza kata za Halmashauri ya wilaya ya Chunya kama Madiwani
Madiwani hao wametoa kauli hiyo leo 20.1.2026 baada ya kuhitimisha mafunzo elekezi kwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Usungilo uliopo jijini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Kelvin Nshinshi aliwataka madiwani wote wa Chunya kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani tayari wamepata uelewa wa namna ya kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao kwani wananchi waliwaamini na waliwachagua kufanyakazi kwa niaba yao.
“Sasa tumepata mafunzo yanayotuongoza kuwatumikia wananchi waliotuamini katika nafasi za udiwani katika kata zetu, kazi iliyobaki ni kuwatumikia wananchi wa Chunya waliotuamini kwa kazi hii ya Udiwani” Alisema Mhe Nshinshi
Naye Diwani wa kata ya Chokaa Mhe Joshua Mlambalala amesema namna kupitia Semina waliyopatiwa yamewasaidia kutambua vyema majukumu yao, mipaka yao ya utendaji lakini pia yamewasaidia kuwapata dira ya namna ya kuongoza kata zao tofauti na fikra za awali walizokuwa nazo kuhusu nafasi na majukumu ya Diwani katika utekelezaji wa Majukumu
“Kupitia Mafunzo haya sasa nimeelewa kwamba kazi ya Udiwani ni kuwatumikia wananchi ikiwa ni Pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yetu jambo ambalo awali sikufikiri hivyo wakati wa Kampeni n ahata kabla ya semina hii” Alisema Mhe Mlambalala
Mafunzo elekezi kwa Madiwani wa Halmashauri ya Chunya yametolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya waziri Mkuu Pamoja na taasisi nyingine lengo likiwa ni kutoa mwongozo wenye nia ya dhati kwa Madiwani kusimamia utekelezaji wa Miradi katika maeneo wanayotoka bila kuwa na migogoro wala misuguano miongozi mwa wananchi na viongozi wao
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.