Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Kelvin Nshinshi amewataka Madiwani wazoefu na wapya kwa Pamoja kupokea mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa majukumu yao katika nyadhifa zao walizoaminiwa na wananchi huku akiwakumbusha kwamba uzoefu wa miaka uliopita uwekwe pembeni ili kupokea maelekezo mapya
Ametoa rai hiyo leo tarehe 19.1.2026 kwenye ukumbi wa mikutano Usungilo Mbeya wakati wa Mafunzo ya Madiwani ambayo yanatolewa na wataalam kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa huku mafunzo hayo yakikusudiwa kuhusisha mada mbalimbali zikiwepo maadili ya madiwani, bajeti na amambo mengine mengi
“Madiwani wazoefu naomba sana, ule uzoefu uliokuwa nao uuache pale mlangoni, ukiingia hapa ukumbi sisi sote yaani madiwani wazoefu na sisi wapya sote tusikilize, tufuatilie na tuwe makini ili tupate ujuzi wa Pamoja utakaotusaidia kutekeleza majukumu yetu huku kwenye kata zetu tulikoaminiwa na wananchi wetu” Amesema Mhe Shinshi
Mratibu wa Mafunzo kutoka OWM-TAMISEMI Bi. Yustina Bubinza kwa niaba ya wakufunzi wote amewataka Madiwani wote kuwa tayari kupokea mafunzo hayo huku akiwataka kuwa huru kuuliza na kutoa maoni ili kuendelea kuboresha zoezi la ujifunzaji kama ilivyokusudiwa kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kutukumbusha Zaidi wakati wa utekelezaji wa Majukumu
Mkuu wa Idara ya Utumishi na utawala wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Jumanne Chaula kwaniaba ya Mkurugenzi mtendaji amewapongeza Madiwani wote walioaminiwa na wananchi na Serikali kwa ujumla wake kuongoza kata hizo hivyo ameahidi ushirikiano mkubwa wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao yote kwa kipindi ambacho watakuwa wanaongoza kata zao
Naye Diwani wa Kata ya Mamba Mhe Ramadhan Shumbi ambaye ameteuliwa na wanasemina kuwa mwenyekiti wa Mafunzo amesema mafunzo hayo yatawasaidia Madiwani kutambua majukumu yao na kutekeleza ipasavyo lakini pia Mafunzo yataondoa mivutano isiyo ya lazima ya viongozi na wananchi wake au viongozi kwa viongozi wao kwa wao
Mafunzo kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya yanafanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Usungilo uliopo jijini Mbeya yakitarajiwa kuongeza uelewa kwa madiwani wote wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya tayari kutekeleza majukumu waliyoaminiwa na wananchi wao

Bi Yustina Bubinza Mratibu wa Mafunzo kutoka OWM TAMISEMI akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya kuongeza uwezo na utendaji

Mkuu wa Idara ya Utumishi na utawala wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Jumanne Chaula akizungumza na wanasemina (Madiwani) wakati wa ufunguzi wa Mafunzo

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakiwa wanafuatilia maelekezo na mafunzo kutoka kwa wakufunzi wao

Mhe Ramadhan Shumbi diwani wa kata ya Mamba na Mwenyekiti mteule wa Mafunzo akizungumza na wajumbe wa Semina mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.