Mkuu wa Wilaya ya Chunya SACI, Mbaraka Alhaji Batenga ametoa rai kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kutumia vyombo vya habari ikiwemo redio , television pamoja na simu za mkononi kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu mfuko wa Bima ya Afya kwa wote kwani kwa kufanya hivyo wananchi wengi watafikiwa hiyo ikiwa ni adhima ya serikali ya kuhakikisha kila Mwananchi anakuwa na Bima ya Afya.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 07/01/2026 wakati wa kikao cha kamati ya afya ya Msingi (PHC) kilichoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya bima ya Afya kwa wote.
“Wakati umefika sasa tumieni na vyombo vya habari mkotoe elimu huko ili muweze kuwafikia wananchi wengi , lakini pia hata kutumia simu za mkononi kutuma ujumbe kuhusu Bima ya Afya kwa wote kusudi elimu hiiweze kuwafikia wananchi wengi Zaidi.” Amesema SACI Batenga
Aidha SACI. Batenga emeongeza kuwa ofisi yake imenunua simu maalumu kwaajili ya kupokea malalamiko mbalimbali ya Wananchi ambapo namba za simu hiyo zitawekwa katika kila taasisi na ofisi zinazotoa huduma kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na Hospital ya Wilaya ya Chunya ili kutatua kero za Wananchi kwa wakati na kuboresha upatikanaji wa huduma.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dr Zuberi Mzige ameahidi katika kikao hicho kuendelea kushirikiana na Mfuko wa Bima wa Taifa kutoa elimu katika mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi za dini na taasisi zingine ili kuwawezesha wanachunya kuwa na ufahamu juu ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote , lakini pia ameahidi kushughulikia changamoto mbalimbali za watoa huduma ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wananchi pasipo Malalamiko
Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mbeya Ndugu Nicholaus Mwangomo ameeleza mambo mblimbali yanayohusiana na Bima ya Afya kwa wote ikiwa ni pamoja na huduma mbalimbali , gharama za bima ya Afya kwa wote , vitita mbalimbali vya huduma , namna ya kujisajili pamoja na mambo mengine mengi.
Wakizungumza kwa niaba ya wajumbe wengine ndugu John Gwimile, Steven Sungura , Mjanaeli Salehe wamehoji mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushiriki wa maduka ya dawa ya watu binafsi, uwezeshwaji wa wazee, garama za Bima ya Afya kwa wote kwa watu wa hali ya chini na mambo mengine mengi ambayo yote yalipatiw majibu.
Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi kimehusisha kamati ya usalama, wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi za dini, taasisi za umma na taasisi binafsi na wawezeshaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Mkuu wa Wilaya ya Chunya SACI. Mbaraka Alhaji Batenga akizungumza na wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wakati wa kikao cha kuwajengea uwezo juu ya bima ya Afya kwa wote kilichoketi katika ukumbi wa Mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dr Zuberi Mzige akijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Afya ya Msingi.
Msimamizi wa Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF) Ndugu Nicholaus Mwangomo akiwajengea uwezo wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi juu ya Bima ya Afya kwa wote katika Ukumbi wa mikutano wa Sapanjo.

Wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali kutoka kwa Mwezeshaji juu ya Bima ya Afya kwa wote katika ukumbi wa Mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.