Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wakili Athumani Bamba ameitaka kamati ya usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ngazi ya kata kuhakikisha wanasimamia vyema urejeshwaji wa mikopo hiyo unaotelewa kwa wanawake , vijana na watu wenye ulemavu ili kuwezesha wananchi wengi kunufaika na mikopo hiyo
Hayo ameyasema leo tarehe 30/12/2025 wakati wa kikao kazi cha kamati ya mikopo ngazi ya kata kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Mwanginde Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kikijumuisha watendaji wa kata ambao ndio wenyeviti na Maafisa maendeleo ya jamii ambao ni Makatibu wa kamati hiyo
Aidha Wakili Bamba meongeza kuwa kutakuwa na motisha kwa wajumbe ambao watatekeleza majukumu yao vizuri hususani kusimamia urejeshwaji ya mikopo hiyo kwa wakati uliopangwa kwani kwakufanya hivyo kutasaidia kuongeza morali ya ufwatiliaji wa mikopo hiyo na kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo hiyo .
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Bi Marietha Mlozi amesema kuwa moja ya majukmu ya kamati hiyo ni ni pamoja kupokea, kujadili na kuchambua maombi ya mikopo iliyopokelewa,kufanya tathimini ya vikundi vilivyowasilisha maombi ikiwa ni pamoja na kuvitembelea na kuvikagua , kufanya fwatiliaji wa marejesho ya mikopo hiyo na majukum mengine .
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Idara ya utawala ndugu Jummanne Chaula amesema kuwa Mkurugenzi ametoa vitendea kazi ili kurahisisha utendaji kazi wa idara ya maendeleo ya jamii ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa vikundi vyenye uhitaji wa mikopo hiyo lakini pia kuhakikisha wanafuatilia urejeshwaji wa mikopo hiyo kwa wakati kwa kushirikiana na kamati ya mikopo ngazi ya kata ili kuwawezesha na watu wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo ya asilimia 10.
Naye Mkuu wa kitengo cha ukaguzi ndugu Herbeth Matugwa amesema kuwa mikopo ya asilimia 10 ni sehemu ya miradi ya serikali kama ilivyo miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri Hivyo kama wajumbe wanapaswa kusimamia na kutimiza majukum yao ili kuhakikisha mikopo inarejeshwa kwa manufaa ya Halmashauri na wanachunya kwa ujumla
“Miradi yote inayotekelezwa kwenye kata usimamizi wake uko kwenu , hii mikopo inayotolewa ni sehemu ya miradi ya serikali kama ilivyo miradi mingine ya Shule , zahanati na miradi mingine hivyo mkasimamie majukum yenu vizuri kuhakikisha mikopo inarejeshwa ili kuiepusha Halmashauri dhidi ya hati chafu” amesema Matugwa .
Wakizungumza kwa niaba ya wajumbe wengine Ndugu Egitho Bilali Mtendaji wa kata ya Makongolosi Bi Nasra Mkupete Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Mbugani wamesema kuwa uwepo wa kamati hiyo ya mikopo ngazi ya kata utarahisisha kwa kiasi kikubwa ufwatiliaji wa marejesho ya mikopo hiyo lakini pia kuwepo kwa motisha kutaongeza chachu katika ufuatiliaji na urejeshwaji wa mikopo hiyo.
Kikao hicho cha kamati ya mikopo ngazi ya kata ni mwendelezo wa vikao vungine vitakavyokuwa vikifanyika mara kwa mara kwaajili ya kufanya tathimini juu ya utekelezaji wa majukum ya kamati hiyo sambamba na kufanya tathimini ya urejeshwaji wa mikopo ya aslimia kumi 10 inayotolewa kwa vikundi vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu pamoja na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinzokuwa zimejitokeza wakati wa ufuatiliaji wa mikopo.

Kaim Mkurugenzi Wakili Athuman Bamba akizungumza na kamati ya mikopo ngazi ya kata juu ya mikakati ya ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mkuu wa idara ya Utawala akisisitiza juu ya matumizi ya vitendeakazi kwaajili ya kuhakikisha vikundi vinapata mikopo na mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati.

Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Ndugu Herberth Matungwa akiitaka kamati kusimamia urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10 kama inavyosimamiwa miradi mingine ya maendeleo wakati wa kikao cha kamati ya mikopo ngazi ya kata kilichoketi ukumbi wa Mwanginde.

Mtendaji wa kata ya Makongolosi Ndugu Egitho Bilali ambae ni mwenyekiti wa kamati ya mikopo ngazi ya kata akichangia juu ya suala la kupata orodha ya vikundi na hali ya urejeshwaji wa mikopo mpaka sasa pamoja na suala la motisha kwa wajumbe wa kamati hiyo

Wajumbe wa kamati ya mikopo ngazi ya kata wakiendelea kufuatilia agenda za kikao katika ukumbi wa Mikutano wa Mwanginde Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.