Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Kelvin Jackson Nshishi amewaasa Madiwani na watalam wa Halmashauri kufanya kazi kwa weledi na bidii katika kuwatumikia wananchi wa chunya ikiwa ni pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo sambamba na kutatua kero mbalimbali za Wanachunya.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 2/12/2025 wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kwa mwaka 2025/2026 kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Nitoe rai kwa wataalamu wote na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kufanya kazi kwa bidii bila kulegalega huku mkisimamia misingi ya utumishi wa umma kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawatendea haki wananchi wetu wa Chunya “. Amesema Mhe.Nshishi
Aidha Mhe. Nshishi na baraza lake ameahidi kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na miundombinu ya afya , elimu , kilimo,madini, na miundo ya barabara ambapo amesema kuwa mitambo ya kutengeneza bararara itakapo kamilika atahakikisha barabara zote zinafunguli ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ndugu Anakleth Michombero ambaye ni katibu tawala Wilaya ya Chunya amewataka waheshimiwa madiwani kwenda kufanya kazi kwani uchaguzi umeshapita kilichobaki na kwenda kufanya mikutano , kusikiliza na kutatua kero za Wananchi na serikali iko bega kwa bega kutoa ushirikiano.
Naye ndugu Noel chiwanga akitoa salam za Chama cha mapinduzi ametao rai kwa madiwani kuwa watu wahekima na kutoa huduma kwa wananchi wao lakini pia ameendelea kuwasisitiza watalamu wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya kutumia utalamu wao kuwahudumia wananchi Ili kuijenga chunya kimaendeleo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Tamimu kambona ametoa mrejesho kwa baraza la madiwani kwa yale mambo ambayo waliyaacha hayajakamilikwa kuwa kwa sasa yametekelezwa kwa asilimia mia sambamabana kuendelea kufanya vizuri katika kukusanya mapato.
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka amesema kuwa jukum kubwa ni kuendelea kukusanya mamapto na kuhakikisha mapato yayo yanakwendenda kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo huku akitoa kwa wanachunya kuendelea kuilinda Amani kwani pasipo Amani hakuna maendeleo yanaweza kufanyika hivyo wananchi wote waaswa kwendelea kuilinda na kuidumisha Amani.
Ndugu zangu tunayafanya haya kwasababu tunaamnai, sisi tuliopo hapa twendelea kulinda na kudumissha Amani, tukapeleke ujumbe kwa watu wengine kuidumisha Amani tukakemee kwa nguvu kubwa , tukatae na kujiepusha na uvunjifu wa Amani kwani bila kuwa na Amani yote tuliyo panga kuyafanya hayawezi kutimia pasipo kuwa na Amani “ amesema Mhe. Masache
Kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kimeenda sambamba na kuapishwa kwa madiwani, kuchagua mwenyekiti na makam mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na kupokea taarifa ya utekeleza wa shughuli mbalimbali zilizottekelezwa kipindi ambacho madiwani hawakuwepo.

Mwenye kiti wa Halmashauri ya WIlaya ya Chunya Mhe.Kelvin Jackson Nshishi akitoa rai kwa watalam na madiwani kufanya kazi kwa weledi wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sapanjo.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ndugu Noel Chiwanga akiwasisitiza watalam kutumia utalam wao kuwasaidia wananchi

Mbunge wa jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka akitoa msisitizo kwa wananchi kuilinda na kuidumisha amani wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kilichofanyika ukumbi wa Sapanjo.

Waheshimiwa madiwani wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa Halmashauri wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.