Mbunge wa jimbo la Lupa Mhe. Masache kasaka kwa kushirikiana na viongozi wa dini na serikali Wameendelea kusisitiza suala la Amani kama ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi kwani shughuli nyingi za kiuchumi na membo mengine mengi yanatendeka panapokuwa na Amani, pasipo Amani hakuna maendeleo na hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika.
Msisitizo juu ya Amani umetolewa leo tarehe 04/12/2025 wakati wa kikao cha viongozi wa dini , na vionngozi wa serikali kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Tuendelee kuiombea nchi yetu ili Amani iweze kutamalaki na ili Amani iweze kutamalaki tunawategemea sana ninyi viongozi wetu wa dini,niwaombe sana viongozi wangu wa dini tunapopata nafasi ya kutoa mnahubiri kwenye idada au mawaidha jambo la Amani tuendeleee kusisitiza tulipe kipaumbele vurugu tuzikatae kwani huo sio utamaduni wetu” Amesema Mhe.Masache.
Aidha Mhe. Masache amesema kuwa uvunjifu wa Amani husababisha madhara makubwa sana katika jamii ikiwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu na mali zingine lakini pia hupelekea watu kupoteza maisha hivyo kila mmoja anajukum la kuilinda na kuidumisha Amani na kuendelea kupinga vitendo vya uvunjifu wa Amani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya ndugu Semwano Mlawa ameendelea kuwasihi viongozi wa dini kuendelea kuhubiri Amani na kukemea vitendo vya uvunjifu wa Amani huku akisema msimamo wa serikali ni kuendelea kulinda watu wake na mali zao na kuhakikisha jamii inakuwa salama kwa namna yoyote ile.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Chunya ametoa rai kwa viongozi wa dini kwendelea kuhubiri Amani kwani hakuna mbadala wa Amani Amani inapotoweka hakuna mtu anaeweza kubaki salama kila mmoja anaathirika kwa namna moja au nyingine hivyo tuendelea kulinda na kudumisha amani.
“Hakuna mbadala wa Amani ndugu zangu hata kama wewe ni billionea,ulikuwa na cheo kikubwa lakini pasipo Amani nafasi hizo zote zinapotea athari za uvunjifu wa Amani zinzathiri kila mmoja wetu kwani hakuna shughuli zinazoweza kufanyika , husababisha mfumuko wa bei za bidhaa na mambo mengine mengi hizo ndizo athari za uvunjifu wa Amani” amesema Chiwanga
Mchungaji wa kanisa la TAG Mch.Maxwel Mwendampapa na Mchungaji Luka Mdoo wa kanisa la morovian kwa niaba ya wachungaji wengine wamesema kuwa wao kama viongozi wanahubiri Amani na kulaani vikali vitendo vya uvunjifu wa Amani kwani ili taifa liendeleee linahitaji Amani na wao kama viongozi wa dini wataendelea kuiombea na kuihubiri Amani katika nchi ya Tanzania kwani kanisa linapenda Amani, upendo na umoja.
Naye shehe Abdul Jambila akiwawakilisha mashehe wengine ametoa rai juu ya matumizi ya mitandao na kuwaomba viongozi wa dini kuwaambia waumini wao kuwa makini na maudhui ya mitandaoni huku akiendelea kusisitiza wao kama mashehe wataendelea kutoa mawaidha ya amni na kuombea Amani ya taifa la Tanzania na kuwaombea viongozi ili amaniiendelee kutamalaki.
Kikao cha Mhe Mbunge na viongozi wa dini na serikali ni mwendelezo wa kuendelea kusisitiza juu ya kuilinda na kudumisha Amani, msisitizo huu umeendelea kutolewa kutokana na uvunjifu wa Amani uliotokea kipindi cha uchaguzi na kusababisha madhara makubwa katika jamii
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.