SHIRIKA lisilo la kiserikali la Child Support Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Christian Blind Mission wamekabidhi msaada wa baiskeli {Viti Mwendo} 5 za walemavu katika shule ya msingi Kibaoni halmashauri ya wilaya ya Chunya.
Msaada huo umelenga kuwawezesha wototo wenye ulemavu kuweza kukabiliana na changamoto zinazo wasababisha wasipate Elimu kwa ufasaha.
Akikabidhi msaada huo leo wenye thamani ya milioni 2.2 Mkurugenzi mtendaji wa Child support Tanzania Bi. Noelah Msuya amesema wao kama shirika wamejikita kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu katika mfumo wa Elimu jumuishi.
Amesema nia yao kubwa ni kuhakikisha wanaondoa vikwazo vinavyo wasababisha waototo wenye ulemavu wasipate elimu kwa ufasaha
“Nia yetu kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu katika mazingira salama na yenye ubora” alisema Bi Noelah Msuya Mkurugenzi mtendaji wa CST.
Vile vile shirika la Child support Tanzania limekuwa likitoa elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu ulinzi na haki za watoto
Bi Noelah Msuya amewataka wazazi wanaopata elimu kuhusu haki za watoto kuhakisha wanaeple elimu hiyo kwa jamii ili kuhakikisha watoto wanakuwa katika mazingira salama .
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka leo amefungua mafunzo ya Mgambo katika tarafa ya kipembawe Kata ya Lupa kijiji cha lupa tingatinga Wilayani humo, jumla ya wana mgambo 84 wameanza mafunzo, pamoja na mambo mengine watajifunza uzalendo, utawala na usalama wa raia.
Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa Robo ya Nne
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.