Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Wakili Athumani Bamba amezitaka idara mtambuka zinazohusika na musuala ya lishe kuhakikisha zinatenga bajeti ya shughuli za lishe katika idara na kuhakikisha kila shughuli ya lishe iliyopangwa kutekelezwa na idara husika inatekelezwa kwa wakati uliokusudiwa
Kauli hiyo ameitoa leo 6/2/2025 wakati wa kikao cha kamati ya lishe robo ya pili kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jingo jipya la utawala (Mwanginde).
“Nendeni mkazingatie na mkatekeleze yale yote yanayotakiwa kutekelezwa, mkatenge bajeti ya shughuli za lishe zinazotakiwa kutekelezwa kwenye idara zenu kwasababu suala la lishe ni mkataba hivyo mkafanyie kazi mapungufu yote na yale yanayotakiwa kutekelezwa yakatekelezwe”amesema wakili Bamba.
Naye Kaim Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala amesema kuwa kitengo cha lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026 wametenga bajeti kwaajili ya mashine za kuongeza virutubishi kwenye nafaka ambapo kata tano zitanufaika, Kata hizo ni Makongolosi, Lupa, Chokaa , Ifumbo na Chalangwa. Lengo ni kutatua changamoto ya lishe pamoja na utapiamlo.
Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Nerberth Gavu ametoa rai kwa idara mtambuka zinazohusika na masuala ya lishe kutenga bajeti za shughuli za lishe na kuonesha zimetenga kiasi gani , na ziendane na uhalisia wa shughuli zinayotekelezwa .
Katika kikao hicho idara mbalimbali zimewasilisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya pili ambapo shughuli mbalimbali zimetekelezwa ikiwa ni pamoja na kuhamasisha jamii kulima mazao lishe, kutoa elimu kwa kina mama wajawazito na wenye watoto, kufuatilia utoaji wa chakula katika shule za Msingi na Shule za Sekondari, kuhamasisha ufugaji wa wanyama wadogo wadogo majumbani kwaajili ya chakula na shughuli zingine.
Kikao ch kamati ya lishe robo ya pili kimehusisha idara ya Maendeleo ya jamii, kilimo na Mifugo, Afya, mipango na uratibu, utumishi, elimu msingi na idara ya elimu sekondari ambapo taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe zimewasilishwa na idara hizo pamoja na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu suala la lishe
Kaimu Afisa Lishe Wilaya ya Chunya ndugu Saimoni mayala akielezea kadi alama za hali ya lishe Katika kikao cha kamati ya lishe robo ya pili kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri (Mwanginde hall)
Kaimu Mkuu idara ya mipango na uratibu Ndugu Nerbert Gavu akitoa msisitizo juu ya utengajio wa bajeti kwa shughuli za lishe kwa idara mtambuka zinazotekeleza masuala ya lishe
Daktari wa mifugo Wilaya ya Chunya Dkt Benedicto Matogo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shuguli za lishe za idara ya kilimo na mifugo kwenye kikao cha kamati ya lishe robo ya pili.
Wajumbe wa kamati ya lishe Wilaya ya Chunya wakiendelea kufuatilia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za lishe wakati wa kikao cha kamati ya lishe robo ya pili kilichoketi ukumbi wa mikutano wa Halmashauri (Mwanginde Hall)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.