Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Zuberi Homera ameridhishwa na matumizi ya fedha ya ujenzi wa shule ya sekondari Nkung’ungu huku akiahidi serikali kuleta fedha ya ziada kwaajili ya kujenga mabweni ya wanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumza leo Februari 10, 2025 Mhe. Homera amesema ameona thamani ya fedha kwenye ujenzi wa shule ya sekondari Nkung’ungu ambayo imejenga vyumba vya madarasa nane na miundombinu mingine kwenye shule hiyo.
“Shule hii italeta maendeleo hapa Nkung’ungu nawapongeza wananchi waliojitolea kujenga shule hii, na nimeambiwa hapa kuwa kuna wanafunzi thelathini na moja ambao wamechaguliwa lakini bado hawajaripoti, nataka mpaka ikifika tarehe 15 mwezi Machi, 2025 wanafunzi hawa wawe wameripoti shuleni” amesema Mhe. Homera.
Mhe. Homera amesisitiza kuwa endapo wanafunzi hao hawataripoti katika kipindi hicho hatua zaidi zitachukuliwa huku akimtaka mkuu wa shule ya sekondari Nkung’ungu kuwapokea wanafunzi hao hata kama hawana sare za shule.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mhe. Bosco Mwanginde amemuleza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuwa, ujenzi wa shule hiyo ulikuwa na changamoto kadhaa ikiwemo wananchi kutaka shule hiyo ijengwe kwenye eneo jingine tofauti na ilipoamuliwa awali(Nkung’ungu) huku akitaja kuwa hizo zilikuwa ni vuguvugu za vyama vya siasa na wanasiasa ambapo kwasasa changamoto hii imekwisha.
Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya shule ya sekondari Nkung’ungu Afisa elimu kata Nkung’ungu Mwalimu Sophia Mgumba amesema shule hiyo imejenga madarasa nane, ofisi mbili, maabara tatu, jengo moja la tehama, mkataba moja, matundu kumi ya vyoo vya wasichana, matundu kumi ya vyoo vya wavulana pamoja na kichomea taka.
“Tulipokea fedha tarehe 26 Juni 2024 kaisi cha Tsh shilingi Milioni 583, pesa iliyotumika mpaka sasa ni milioni 433, na bakaa ni mil 149” amesema Mwalimu Mgumba.
Mwalimu Mgumba aliongeza kuwa, malengo ya mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Nkung’ungu ni kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, ambapo mpaka sasa tayari wameanza kusoma huku wanafunzi waliochaguliwa wakiwa ni 83, wasichana 34, wavulana 49. Wanafunzi walioripoti ni 48, wasichana 25 na wavulana 23.
Malengo mengine ni kupunguza umbali na utoro. Changamoto kubwa kwenye ujenzi wa shule ya sekondari Nkung’ungu kuwa ni mfumo wa manunuzi wa (NeST) uliochelesha mradi kuanza na kukamilika kwa wakati uliopangwa amesema Mwalimu Mgumba.
Mkuu wa Mkoa Mbeya, Mhe. Juma Zuberi Homera akikagua maendeleo ya ujenzi wa wa shule ya Sekondari Nkung’ungu iliopo Wilaya ya Chunya.
Muonekano wa maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Nkung’ungu ukiwa kwenye hatua ya mwisho ya ukamilishwaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akipokelewa na viongozi pamoja na kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari Nkung’ungu baada ya kuwasili katika shule hiyo kwaajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi.
Baadhi ya wananchi, wanafunzi na viongozi wa shule ya Sekondari Nkung’ungu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera alipokuwa akihutubia wananchi hao mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Nkung'ungu.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.