MKUU WA MKOA WA ARUSHA MH. MRISHO GAMBO AKIONGEA NA MAAFISA HABARI, MAWASILANO SERIKALINI
kuanzia tarehe 12-16 Machi kilifanyika kikao kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini. ambapo Hotuba, Mada na Mijadala Pamoja na Maazimio Mbalimbali Viliwasilishwa.
ifuatayo ni hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Akimkaribisha Mgeni Rasmi wa Kikao hicho Mh. Waziri wa Habari, Ndg. Harisson Mwakyembe; HOTUBA YA KATIBU MKUU.pdf
UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI KILICHOFANYIKA UKUMBI WA HAZINA NDOGO MJINI DODOMA MACHI 13-17, 2017.
1. Kuanzishwa mfumo wa kuweka malengo na upimaji wa Taasisi katika eneo la mawasiliano.
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo iliandika barua yenye Kumb NA FA/238/292/01B/21 ya tarehe 27 Machi, 2017 na
kutumwa kwa Wizara zote, Wakala na Idara zinazojitegemea pamoja na Taasisi zote za Serikali.
Barua hiyo ilieleza umuhimu wa taasisi kutekeleza malengo ya kitaifa ya Mawasiliano pamoja na Maazimio mengine ya Kikao
kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini cha mwaka 2017.
Aidha, kufuatia barua hiyo, Ofisi ya Rais TAMISEMI iliandika barua yenye Kumb Na AB.156/174/01 ya tarehe 9, Mei, 2017
kwenda kwenye Mikoa na Halmashuri zote nchini ikiambatanishwa na malengo ya Kitaifa ya mawasiliano yaliyopitishwa wakati
wa kikao kazi pamoja na maazimio kwa utekelezaji.
Wizara zote zilipewa taarifa kuwa utekelezaji wa Malengo utaanza kupimwa rasmi kuanzia Julai 2017.
Baadhi ya Wizara zimekuwa zikiwasilisha taarifa hizo Idara ya Habari – MAELEZO kila mwezi ambapo pia kumekuwa na Mikutano
kati ya Msemaji wa Serikali na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara. Taarifa zinaonyesha bado utekelezaji
wa Malengo ya Kitaifa ya Mawasiliano sio mzuri.
Hatujapata taarifa za utekelezaji kutoka kwa Maafisa Mawasiliano wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi
nyingine za Serikali.
Tathmini ya Wizara zilizotekeleza malengo ya Kitaifa na kuwasilisha taarifa zao inaonyesha waliofanya vizuri na wale ambao
hawajawasilisha taarifa zao.
2.Maafisa Habari/Mawasiliano kutekeleza Sheria ya Huduma ya Habari na Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa na Kanuni zake kwa
kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara na kwa wakati.
Idara ya Habari MAELEZO imekuwa ikifanya mikutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kitaifa,
Msemaji Mkuu wa Serikali amekuwa akishirikisha Wizara na Taasisi husika kupata taarifa na takwimu katika masuala husika.
Taarifa hizo zimekuwa zikitangazwa kupitia Radio, Televisheni, Magazeti na Mitandao ya Kijamii ikiwemo Blogs, Maelezo TV,
Facebook, Twitter ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Makundi mbali mbali ya Instagram.
Aidha, Ofisi ya Rais TAMISEMI iliandika barua yenye kumb. Na. EB.151/297/104 ya tarehe 06 April, 2017 kuwataka Wakuu wa
Mikoa kuhakikisha kuwa Tovuti zote za Mikoa na Halmashauri zinakuwa na taarifa za kutosha zinazotolewa kwa wakati.
Barua hiyo imeelekeza mikoa kuhakikisha kuwa Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri wanashirikishwa katika shughuli zote
za mikoa na halmashauri kwa kuingia katika vikao vyote muhimu ili kuwa na uelewa mpana wa shughuli za mkoa au halmashauri
husika na kutoa ushauri utakaofanikisha ofisi hizo kutoa mawasilia kwa umma kwa ufanisi.
Tathmini fupi tuliyoifanya inaonyesha Wizara, Mikoa na Halmashauri nyingi zinafanya vizuri kwenye eneo la kuweka taarifa
kwa wakati kwenye tovuti.
Hata hivyo, bado kuna changamoto kwa baadhi ya taasisi katika kuweka taarifa kwa wakati kwenye Tovuti zao.
3. Maelekezo yatolewe kwa taasisi zote kutenga bajeti na kununua vitendea kazi kwa ofisi za Mawasiliano.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI walitoa maelekezo mahususi kuhusu
suala la Taasisi kutenga bajeti za kununulia vitendea kazi kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini. Maelekezo hayowakati wa
uzinduzi wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri mjini Dodoma mwezi machi 2017 mara baada ya Kikao Kazi. Maelekezo hayo
yalisisitizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI katika barua yake yenye Kumb. Na. EB.151/297/104 ya tarehe 06
April, 2017.
Aidha, aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika kipindi 2016/2017 akiwa katika ziara zake Mikoani
alisisitiza kila Mkoa na Halmashuri kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kuwanunulia vifaa Maafisa Habari na Mawasiliano
Serikalini.
Bado kuna changamoto ya baadhi ya ofisi kutokuwa na vitendea kazi pamoja na watendaji wa ofisi za Mawasiliano kutoruhusiwa
kuingia kwenye vikao vya maamuzi. Wapo waliojitokeza kueleza hali halisi.
4. Mikoa iandae ratiba za mikutano na vyombo vya Habari kwa Halmashauri, Manispaa , Majiji, Miji na Taasisi zilizoko
katika mkoa husika.
Wizara ya Habari iliandika barua yenye Kumb NA FA/238/292/01B/21 ya tarehe 27 Machi, 2017 na kutumwa Ofisi ya Rais
TAMISEMI. Barua hiyo ilieleza kuhusu umuhimu wa mikoa kutekeleza maazimio ya Kikao kazi cha mwaka 2017 likiwemo suala la
kuitaka Mikoa kuandaa na kutekeleza ratiba ya mikutano na Vyombo vya Habari.Hatuna taarifa za utekelezaji wa azimio hili.
5. Maafisa Habari wa Taasisi, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa waruhusiwe kuingia vikao vya maamuzi
Wizara ya Habari iliandika barua yenye Kumb Na. FA/238/292/01B/21. Kufuatia barua hii Ofisi ya Rais TAMISEMI
waliandika barua yenye Kumb. Na. EB 151/297/01/104 ya tarehe 06 April 2017 kwenda kwa Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara
ili Maafisa Mawasiliano wa Sekretariet za Mikoa na Serikali za Mitaa wapatiwe Vitendea kazi vikiwemo Kamera, Kompyuta
mpakato, Inteneti na pia waruhusiwe kuingia kwenye vikao vya menejimenti.
Baadhi ya Maafisa Habari wa Mikoa wanaingia kwenye vikao vya Menejimenti. Mikoa iliyothibitisha kuwa Maafisa Habari wake
wanahudhuria vikao vya Menejimenti ni Simiyu, Pwani, Arusha, Shinyanga, Lindi, Dodoma, Songwe na Kigoma.
Bado kuna changamoto ya baadhi ya Maafisa Habari wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoruhusiwa
kuingia kwenye vikao vya Menejimenti.
Waziri Wa OR-TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo(wa pili kulia) akiwa na katibu mkuu wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi(mwenye koti la Pinki), na Msemaji wa Serikali Ndg. Hussein Abas
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.