Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Lupa Wakili Athuman Bamba, amewataka walioteuliwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kufanyakazi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura awamu ya pili kufanya kazi kwa weledi, umakini na ufanisi wa hali ya juu kwani Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imewaamini na ina Imani watatekeleza kazi hiyo kwa maslahi ya Taifa la Tanzania
Ametoa kauli hiyo mapema leo 29/04/2025 wakati akifungua mafunzo ya waandishi wasaidizi na waemdesha vifaa vya Bayometriki wanaotarajiwa kuongoza zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili linalotaraji kuanza tarehe 1/5/2025 na kuhitimishwa tarehe 7/05/2025
“Sasa hivi idadi yetu ni ndogo kuliko ilivyokuwa awali, hivyo ninyi mmeaminiwa sana na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kufanya kazi awamu hii ya Pili, Zingatieni mafunzo haya ili kazi yenu ikawe yenye ufanisi na weledi unaokususdiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi” Amesema Wakili Bamba
Dkt. Theodory Lukas ambaye ni moja kati ya wakufunzi wa Mafunzo hayo amewataka washiriki kutokupuuzia kila kinachofundishwa kwani Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi wanajua umuhimu wa Ninyi kupewa mafunzo haya jambo lililopelekea kuitwa katika mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Mafunzo Mw Isakwisa Kaminyoge kwa niaba ya wanasemina wote amewashukuru wakufunzi waliotumika kutoa mafunzo hayo lakini amewashukuru washiriki kutoa ushirikiano mkubwa wakati wa Mafunzo hayo huku akisisitiza washiriki wote wa Semina kwenda kuyatendea kazi mafunzo hayo watakapokuwa wanatekeleza zoezi la uboreshaji wa Taarifa katika Daftari la Kudumu la mpiga kura awamu ya pili
Jimbo la Lupa linataraji kuwa na vituo ishirini na sita (26) ambapo kata kumi na sita (16) zitakuwa na kituo kimoja kwa kila kata kitakachotumika katika uboreshaji (Ofisi za Kata) wakati kata za Kambikatoto, Mafyeko na Mamba kwa Tarafa ya Kipembawe na Kata za Matundasi Chokaa na Sangambi kwa tarafa ya Kiwanja zitakuwa na vituo viwili kwa kila kata
Mafunzo hayo yametolewa leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) yakiwahusisha maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata, waandishi wasaidiizi ngazi ya vituo pamoja na waendesha vifaa vya Bayometriki huku zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura awamu ya pili likitaraji kuanza rasmi tarehe 01/05/2025 na kutamatika tarehe 07/05/2025
Afisa Tehama Kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ndugu Salim Hassan Mohamed akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata, waandishi wasaidizi wa vituo na waendesha vifaa vya Bayometriki
Wahiriki wa Mafunzo wakila kiapo tayari kwa kazi ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura awamu ya Pili Jimbo la Lupa
Washiriki wakiendelea na mafunzo kwa Vitendo tayari kwa kazi ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura linalotaraji kuanza tarehe 1/05/2025 na kutamatika tarehe 7/05/2025
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.