Waziri wa madini Mheshimiwa Dotto Biteko ameagiza wafanyakazi wa ofisi ya madini wilayani Chunya kusimamishwa kazi wote nakufikishwa katika vyombo vya kisheria kwa kosa la uhujumu uchumi.
Wafanyakazi hao wanashutumiwa kushirikiana na wachenjuaji wa madini kuibia serikali. Katika kikao cha ndani kati ya waziri na wachimbajij pamoja na wachenjuaji, alisema kuwa Chunya inaongoza kwa uwizi na utoroshwaji wa madini ikifuatiwa na Kahama.
Mh. Waziri amesema kuwa serikali kupitia ofisi ya madini imefanya utafiti na kubaini kuwa taarifa ya madini inayoripotiwa serikalini ya kiwango cha madini inayopatikana siyo sahihi ambapo unakuta mtu kapata kilo 1 na gramu 1620 lakini serikalini inaripotiwa gramu208.
Waziri amewaomba watendaji wa serikali na wachimbaji na wote wanaohusika na sekta ya madini kuwa na moyo wa uzalendo kwa nchi yao.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.