ZIARA YA MHESHIMIWA MKUU WA WILAYA YA CHUNYA MH: REHEMA MADUSA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA MIUNDOMBINU.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh.Rehema Madusa leo tarehe 27/11/2017 alikua katika kijiji cha Lupamarket kata ya Ifumbo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja miundombinu ya shule ikiwepo ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Lupamarket. Katika ziara hiyo Mh.Mkuu wa wilaya aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi. Sophia Kumbuli, Kaimu Afisa Elimu msingi Ndg Labrey Urasa Pamoja na kaimu Afisa Tawala wilaya Ndg.Kaisi
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya alikutana Walimu na kamati ya shule ya Msingi Lupamarket ambao walimueleza changamoto wanazokumbana nazo ikiwepo upungufu wa vyumba vya madarasa, Ofisi ya walimu, Nyumba za walimu pamoja upungufu wa walimu. Kuhusu kero hizo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Kaimu Afisa Elimu waliahidi kuendelea kuzifanyia kazi Changamoto hizo.
Mwalimu mkuu shule ya Msingi Lupamarket akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wilaya huku akisikilizwa kwa makini na walimu pamoja na kamati ya shule.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya alikabidhi bati bando mbili (2) ambazo ni sawa na mabati 32 kwa Mkurugenzi Mtendaji wilaya kwa ajili ya ujenzi ya nyumba ya walimu
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Rehema Madusa (kushoto) akimkabidhi bati Mkurugenzi mtendaji wilaya Bi. Sophia Kumbuli
Picha ya Pamoja ya Mheshimiwa Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, Kaimu Afisa Tawala wilaya, Walimu na kamati ya Shule baada ya makabidhiano ya Bati mbele ya Nyumba ya walimu ambayo bado ipo katika ujenzi.
Mheshimiwa Rehema Madusa katikati, Mkurugenzi mtendaji Bi. Sophia Kumbuli kushoto wakiteta jambo na Mwalimu Mkuu shule ya msingi Lupamarket.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya alitoa maagizo yafuatayo:
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.