Zaidi ya hekta 8 za misitu huaribiwa kwa mwaka wilayani Chunya ambapo viongozi mbalimbali wametumia siku ya mazingira Duniani kuwaasa Wananchi kutumia nishati mbadala ili kunusuru Wilaya kugeuka jangwa.
Kauli hizo zilitolewa jana katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambapo Wilaya ya Chunya yalifanyika kijiji cha Soweto Kata ya Kasanga mgeni rasmi akiwa mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ambaye alitumia fursa hiyo kusisitiza kauli mbiu ya siku hiyo Kimataifa iliyokuwa ikisema"Pambana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki na kitaifa ni mkaa ni gharama tumia nishati mbadala".
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa alisema zaidi ya kilometa nane za misitu huharibiwa katika Wilaya ya Chunya na hali hiyo ikifumbiwa macho itasababisha Wilaya kugeuka kuwa jangwa .
Madusa alisema waachane na tabia za kufyeka misitu ovyo kwani watasababisha ukosefu wa mvua na kuharibu vyanzo vya maji,na alitumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji kusimamia Sheria na atakaye kiuka achukuliwe hatua za kisheria mara moja.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi diwani wa kata ya Kasanga Obed Mwangesile alishukuru maadhimisho hayo kufanyika katika Kata yake kwani wananchi wa Kata yake ni miongoni wa wanufaika na mazingira katika kutokana na shughuli za kibinadamu kama kilimo, Ufugaji na Uchimbaji Madini ya dhahabu ambapo alisema kupitia maadhimisho hayo wananchi wamepata elimu ya mazingira.
Awali Ofisa mazingira Wilaya ya Chunya Yohana Ngurukia akielezea uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya Chunya alisema unasababishwa na shughuli za kibinadamu kama uchimbaji madini, uchomaji mkaa na ufugaji mifugo wa kuhamahama ambao husababisha uchomaji misitu wakidai hufukuza adui wasidhuru mifugo.
Ngurukia alisema umefika wakati wa kuachana na matumizi ya nishati ya mkaa badala yake watumie nishati mbadala kama gesi,umeme ili kuokoa misitu iliyobakia.
Aidha kwaupande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Sophia Kumbuli alisema Halmashauri yake itaendelea kuzimamia Sheria ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na kuwataka watendaji wa vijiji wanawahimiza wananchi kufuata Sheria badala ya kuharibu mazingira.
Hata hivyo BI. Sophia Kumbuli alisema kuwa hivi karibuni walindesha mafunzo kwa vikundi vya ujasiriamali kwaajili ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kuanza uzalishaji wa mkaa kwa kutumia taka ambao hautumii nishati ya miti.
Mwenyekiti wa Wachimbaji Mkoa wa Mbeya Leonard Manyesha alisema kupitia maadhimisho haya yeye kama Mwenyekiti atasaidia kuwaelimisha Wachimbaji ili kuhakikisha wanafuata Sheria na kwamba wanapaswa kufuata Sheria ili kuepuka uharibifu wa mazingira.
Alisema Wachimbaji kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuepuka uharibifu wa mazingira kwa kutotirisha maji ovyo kwenye machimbo na kufukia mashimo baada ya machimbo.
Mwisho.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.