Timu ya watumishi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya imechukua Ubingwa kibabe Mchezo wa kuvuta kamba wanaume baada ya kuwafunga nje ndani wapinzani wake wote bila ajizi wakiwepo Da res salaam (DAR CC) huku wakisema tumelipa deni kwa viongozi wetu kwa namna walivyotujali wakati wa maandalizi, wakati wa safari na hata kipindi chote ambacho timu iliko jijini Dodoma
Wakizungumza kwa shangwe na bashasha chini kapteni wa timu ya wanaume kuvuta kamba wamesema tumekamilisha kulipa Deni kwa viongozi wetu iliyobaki Sasa ni nguvu kwa maandalizi ya msimu ujao yaani mwaka 2024
“Mwaka huu kuna tofauti kubwa maana mwaka jana tulifungwa na kutolewa hatua ya makundi laki mwaka huu tumetolewa hatua ya 16 bora na hata aliyetutoa anasimulia kwamba nimeitoa timu, kwenye kamba pia kuzishinda halmashauri zaidi ya mia na hamsini sio shughuli ndogo pia tumepata Mchezo wa kirafiki na sHalmashauru ya Singida ambapo umetoka sare ya magori matatu na hii imetokana na mchezo ambao wilaya ya Chunya tumeonesha ikapelekea Singida kuvutiwa nasi na hatimaye kutuomba mechi” Alisema Ridhiwani Mshigati
Kiongozi wa msafara kwa ujumla ambaye ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii wilaya ya Chunya ndugu Vincent Msolla amesema usikuvu, utii na kusikiliza maelekezo tuliyokuwa tunawapatia wachezaji tulipokuwa tunakaa vikao ndio Siri ya mafanikio ya safari yetu hatimaye ubingwa tumeubeba na kufikia hatua mbalimbali za mashindano kwa michezo mingine
“Mchezo wa kuvuta kamba ni mchezo mgumu kuliko watu wanavyofikiri lakini sisi Chunya tulikusudia kuchukua ubingwa huo na tumezoea maana sio mara ya kwanza na kwenye vikao vyetu tulikuwa nasisitizana kwa tunalo deni la kuwalipa kwa mwajili na ni kuchukua makombe tu. Na kwa mikakati tuliyoiweka mwakani tunachukua pia kombe kwenye mpira wa miguu, netball handball maana hata mwaka huu tumeonesha mabadriko makubwa maana hata tulipotolewa kwenye football watu wengine walikuwa wanashangaa kwa kiwango tulichoonesha”
Chunya imeshiriki michezo ifuatayo
Kuvuta Kamba (Me) Chunya Bingwa
Kuvuta Kamba (KE) Chunya Mshindi wa Tatu
Kurusha Tufe Chunya Dc Mshindi wa tatu
Mchezo wa Draft Chunya Dc Mshindi wa nne
Mpira wa Miguu Tumetolewa 16 bora
Netball tunetolewa hatua ya makundi
Watu wa kazi wakiwa katika jukumu la kuiheshimisha Halmashauri ya wilaya ya Chunya na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla wake huko Dodoma
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.