Serikali wilayani chunya imeanza kuwachukulia hatua za kisheria wazazi ambao hawajawapeleka watoto kuanza masomo ya sekondari kwa wale waliochaguliwa kujiunga katika shule mbalimbali za sekondari wilayani humo.
Mapema Leo wazazi kumi wamefikishwa mahakama ya mwanzo Makongolosi mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi Vensensia G. Ketapo na Hakimu Mkazi Daniel Gugamu kwa tuhuma za kushindwa kutoa mahitaji muhimu chini ya kifungu namba 167 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 Marejeo ya mwaka 2022
Watuhumiwa wote kumi ni wakazi wa Kata ya Matundasi mitaa ya Kisimani na Matundasi A wamekiri kutenda kosa Hilo huku sababu mbalimbali zikitajwa kupelekea wao kushindwa kupeleka watoto wao shule kwaajili ya masomo kwa Ngazi ya elimu ya sekondari.
Kwa Mujibu wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Matundasi ndugu Mashaka Edom Mwanjunga amesema kabla hawajaanza kuwakamata wazazi ambao hawajawapeleka watoto shule ya sekondari Makalla ni wanafunzi 105 kati ya wanafunzi 228 waliokuwa wameripoti shuleni.
Ndugu Mwanjunga amesema baaada ya kuwakamata watuhumiwa hao kumi idadi ya wanafunzi kuripoti shule imeongezeka kutoka wanafunzi 105 ijumaa ya tarehe 20/1/2023 na kufikia 152 leo jumanne tarehe 24/1/2023.
Aidha Mwanjunga amesema Zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha wanafunzi wote 76 ambao bado hawaripoti shule wanaripoti kwani serikali imejenga miundombinu yote inayomuwezesha mwanafunzi kupata Elimu katika shule ya sekondari makalla.
Ikumbukwe hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Mayeka Simon Mayeka aliwaagiza watendaji wa Kata wilayani Chunya kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wazazi ambao bado hawajawapeleka wanafunzi shule
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika Nyakati tofauti tofauti amewataja watendaji kuwachukulia hatua za kisheria wazazi au walezi ambao hawajawapeleka wanafunzi shuleni huku akimwagiza Afisa Elimu sekondari kuhakikisha hakuna michango isiyo ya Lazima ambayo inaweza kuwazuia wazazi kuwapeleka wanafunzi shuleni
Washitakiwa sita (6) wamekidhi vigezo vya dhamana hivyo wapo nje kwa dhamana wakati washitakiwa wane (4) hawajakidhi vigezo vya dhamana hivyo wamerudishwa rumande, kesi hiyo itakuja kwaajili ya kusikilizwa tarehe 3 February 2023.
Baadhi ya wazazi waliofikishwa Mahakamani kwa kushindwa kuwapeleka watoto Sekondari wakitoka katika mahakama ya Mwanzo Makongolosi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.