Hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya Wilaya Mhe.James Mhanusi amewataka watumishi wa kada zote kuendelea kusimamia maadili na kutekeleza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi na kujiepusha na vitendo visivyo vya kimaadili huku wakizingatia misingi ya kutenda haki wawapo kazini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma za utoaji haki kwa wananchi zinapatikana kwa wakati.
Hayo ameyasema leo tarehe 3/2/2025 wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo) yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya 2050: nafasi ya taasisi zinazosimania haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo,”
“Mahakama ya Wilaya ya Chunya tumeendelea kukemea vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kwa watumishi na kukumbushana kuhusu maadili na wajibu wetu tuwapo kazini,lakini pia kuhakikisha huduma za utoaji haki kwa wananchi zinapatikana kwa wakati na kuendelea kusirikiana vema na wadau wote na wananchi kwa ujumla ili kutimiza wajibu huo”. Alisema Mhe. Mhanusi
Vile vile Mhe. Mhanusi amesema kuwa Mahakama imeendelea kusikiliza mashauli mbalimbali na kutoa nakala za hukumu kwa wakati , kusikiliza malalamiko ya wadau na kuyatolea majibu kwa wakati hali inayofanya wananchi kupata haki zao kwa wakati lakini pia inasaidia mahakama kutokuwa na mulundikano wa mashitaka.
Katibu tawala wa Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya amewataka wadau wa mahakama kuendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao na kutenda haki ili kupunguza mrundikano wa majukumu upande mmoja kwani kila taasisi inayosimamia haki ikitekeleza majukumu yake itasaidia kupunguza mzigo wa majukum katika taasisi nyingine .
Naye Mkuu wa Mashitaka Wilaya ya Chunya ndugu Mwajabu Tengeneza amesema kuwa madhumni ya siku ya sheria ni pamoja na kutathimini dhana ya utoaji wa haki na mchango wa kila taasisi inayotoa haki, kutoa elimu juu ya haki kwa jamii na kuwaombea majaji na mahakimu ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kutenda haki kwa hekima na busara.
Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ustawi wa Jamii , jeshi la polisi , takukuru na wadau wengine wameeleza umuhim wa wiki ya sheria kwani imekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali yahusuyo sheria na kuwawezesha wananchi kutambua wajibu na haki zao katika jamii na taifa kwa ujumla.
Kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini huadhimishwa kila mwaka mwanzoni mwa mwezi February ambapo kwa mwaka huu maadhimisho yalitanguliwa na wiki ya sheria iliyoanza tarehe 25/1/2025 katika Wilaya ya Chunya ,uzinduzi wa wiki ya sheria ulifanyika katika kijiji cha Kambikatoko kata ya Kambikatoto na kilele cha maadhimisho kimefanyika leo tarehe 3/2/2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri (Sapanjo) uliopo kata ya Itewe na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, vyama vya siasa wadau wa Mahakama , kwaya kutoka madhebebu mbalimbali na wanafunzi .
Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya Katibu tawala wa Wilaya ndugu Anakleth Michombero amewataka wadau kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu , hayo ameyasema wakati wa kilile cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo).
Shekh Kasimu Issa akiomba dua wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo).
Watumishi wa Mahakama wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu wakati wa kilile cha maadhimisho ya wiki ya sheria Wilayani Chunya.
Viongozi wa Madhehebu mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu wakati wa kiklele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.