Katibu wa kikao cha cha tathimini ya Mkataba wa lishe wilaya akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Athumani Bamba amemwagiza kaimu afisa lishe wa wilaya ndugu Witness Kisukulu kuhakikisha anawaandikia barua watendaji wa vijiji na wakuu wa shule kuwataka wasimamie na kuhakikisha watoto wote wanapata chukula shuleni.
Maagizo hayo yametolewa julai 20/07/2023 katika kikao cha tathimini ya hali ya lishe wilaya ikiwa ni kikao cha robo ya nne (4) kilichofanyika katika ukumbi wa halimashari ya wilaya ya chunya
“Kaimu Afisa lishe wilaya hakikisha unawaandikia watendaji na wakuu wa shule wote barua ipitie kwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya kuwataka wasimamie na kuhakikisha watoto wote wanapata chakula shuleni kusiwepo na watoto ambao hawapati chakula wanapokuwa shuleni ukizingatia kipindi hiki ni kipindi cha mavuno kwahiyo ni kupambana kuhakikisha wazazi wanaleta chakula shuleni”
Mwenyekiti wa kikao ameongeza kuwa watendaji wa vijiji na kata waweke sheria ndogo ambazo zitawasaidia kusimamia suala la ukusanyaji wa chakula shuleni ili kuwawezesha watoto wote kupata chakula na kwa wazazi ambao watakaidi agizo hilo basi sheria ndogo zilizowekwa zitumike kuwachukulia hatua wazazi hao.
Naye kaimu Afisa lishe wa wilaya ndugu Witness Kisukulu amewataka watendaji wa vijiji na kata kuendelea kuwaibua wototo wenye utapiamlo waliopo katika jamii ili wapatiwe matibabu lakini pia kwendelea kutoa elimu ya lishe katika jamii ili kupunguza na kumalikza kabisa tatizo la utapiamlo kmali na udumavu katika jamii zetu’’
“watoto wenye utapiamlo kwenye jamii zetu bado wapo hivyo watendaji tunapaswa kwendelea kutoa elimu ya lishe kuelimisha jamii lakini pia kuibua watoto wenye utapiamlo ili waweze kupata matibabu sambamba na kuhamasisha wakina mama wawanyonyeshe watoto kwasababu garama za utapiamlo ni kubwa”
Aidha afisa elimu awali na Msingi Ndugu Ferd Yona Mhanze ameeendelea kuwasisitiza watendaji wa kata na vijiji kushirikiana na wakuu wa shue kuhakikisha watoto wote wanapata chakula wanapokuwa shuleni na hiyo ni kwa shule zote za halimashuri ya wilaya ya chunya.
‘’Kwa shule zile zenye watoto wenye mahitaji maalumu serikali inawatambua na inawachangia kiasi cha Tsh 12000/= kila mwezi hii inaweza ikatumika kama mchango wake wa chakula kwa mtoto ili kumsaidia mtoto mwenye ulemavu asipate usumbufu wakukosa chakula anapokuwa shuleni’’
Aidha ndugu Semwano Carlos Mlawa akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya halmashauri ya Chunya amezipongeza kata zilizofanya vizuri katika masuala ya lishe kwa mwaka huu na kuwasihi waendelee kufanya zizuri huku akiwataka watendaji wa kata zingine kuhakikisha wanafanya vizuri katika masuala ya lishe kwa mwaka ujao.
Gervas Cosmas Mahellah akizungumza kwa niaba ya watendaji ameomba maagizo ambayo yametolewa kwenye kikao cha kamati ya lishe yaweze kubandikwa katika mbao za matanago za vijiji na kata ili vikao vya halmashauri ya vijiji wanapokuwa wameketi waweze kuingiza na agenda ya chakula mashuleni.
Kikao hicho cha kamati ya lishe kimehudhuriwa na watendaji wa vijiji , watendaji wa kata , afisa elimu awali na msingi, Kaimu mganga mkuu na Kaimu katibu tawala wa wilaya. Kikao hicho kiliambatana na zoezi la ugawaji wa zawadi kwa watendaji wa kata ambao wamesimamia vizuri musuala ya lishe katika kata zao ambapo Watendaji wa kata za Mkola, Lupa na kata ya Nkung’ungu wamepata zawadi
Kaimu Afisa lishe wilaya ya Chunya Ndugu Witness Kisukulu akizungumza katika kikao cha tathimini ya makataba wa lishe cha Robo ya nne ya mwaka 2022/2023 kilichowahusisha watendaji wa kata nai vijiji wa Halmashautri ya wilaya ya Chunya
Mtendaji wa kata ya Matwiga Ndugu Gervas Cosmas Mahellah akichangia mada kwenye kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe cha Robo ya mwaka 2022/2023
Afisa Elimu awali na Msingi ndugu Ferd Yoha Mhanze akifafanua jambo wakati wa kikao cha Lishe Robo ya nne ya mwaka 2022/2023
Afisa tawala wilaya ya Chunya Ndugu Semwano Carlos Mlawa kwa Niaba ya Katibu tawala wilaya ya Chunya akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mtendaji wa Kata ya Mkola Ndugu Steven Ndoni
Wajumbe wa kikao cha tathimini ya Mkataba wa lishe Robo ya nne ya mwaka 2022/2023 wakifuatilia mjadala unaendelea kuhusu kuboresha lishe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.