“Kuanzia tarehe 01/07/2022 fedha zote zinazo kusanywa lazima ziende banki alafu zitatumika zikitoka banki lakini ni lazima ziingizwe kwenye mfumo”.
Haya yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg Tamim Kambona wakati wa mafunzo ya Mfumo wa fursa na vikwazo kwa Maendeleo {O&OD ulioboreshwa}kwa watendaji wa kata pamoja na watendaji wa vijiji.
Walimu wakuu wanajua swala la mfumo, waganga wafawidhi wanajua na wakuu wa vituo vya Afya wanajua hilo sio swala geni na naimani hata watendaji mtakuwa mnafahamu hilo”.
Aidha Tamim aliongeza kwa kusema lengo la serikali ni kudhibiti mapato, kadri serikali inapoona kuna sehemu maboresho yanataikiwa yafanyike inaendelea kufanya maboresho, kwahiyo hayo yanayofanyika nimaboresho.
Hivyo kwa mwaka unaokuja sasa ni lazima ofisi zetu za kata pamoja na vijiji zitumie mfumo wa FASS, na mimi ningefurahi zaidi Afisa Mipango hata miradi inafaa tuipeleke kwenye ngazi ya chini iyonekane huko.
“sitaki kabisa kukaa na miradi hapa halmashauri tunataka miradi yote inayotekelezwa huko fedha zije moja kwa moja kwenu hilo tumelianza hata kule Sangambi Mtendaji anajua”.
Kwa upande wa Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya ya Chunya ndg Nebert Gavu alisisitiza kuwa ule utaratibu wa kukushanya fedha na kuzitumia sasa utaratibu huo mwisho ni juni 30 mwaka huu.
“zilefedha tulizo kuwa tunakusanya tunaita fedha mbichi Ukisha kusanya unatumia sasa hiyo tabia mwisho wake ni mwaka huuitakapofika tarehe 30 juni,kuanzia tarehe 01julai usifanye hiyo tabia tena kusanya fedha weka kwenye akaunti benki zeni Omba malipo”.
Nao washiriki wa mafunzo hayo kupitia kwa mwenyekiti wao Ndg Gervas Mahella Ameupongeza Uongozi wa halmashauri kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yanamanufaa sana kwao.
Tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Mkurugenzi mtendaji wa wilaya wakuu wa Idara na wahusika wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kushauri mafunzo haya ya O&OD kufanyika ilikusudi tuendane na wakati.
“Mifumo ya sasa ni yawakati tupende tusipende hatuweze kupingana na dunia, kila badiliko lazima sisi tuendane nal ilikusudi tuwe sambamba na wengine”. Gervas Mwenyekiti wa watendaji wilaya ya Chunya.
Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya wakiwa katika mafunzo ya O&OD
Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya wakiwa katika mafunzo ya O&OD
Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg Nebert Gavu Akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya O&OD
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya Ndg Vincent Msolla Akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya O&OD kwa watendaji wa kata na Vijiji
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.