Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu mwandamizi wa Uhamiaji Mhe.Mbarak Alhaji Batenga amewataka watendaji wa vijiji kutumia vizuri majina na mahudhurio ya watu wakati wakuaandaa mhitasari mara baabda ya mkutano kufanyika kwa kuhakikisha wanaandika yale yaliyojadiliwa na wajumbe kwenye Mkutano na sio mambo mengine .
Hayo ameyasema April 3, 2024 wakati wa kikao kilichoketi katika kanisa la Pentekoste kijiji cha Ifumbo kata ya Ifumbo cha kusuluhisha mgogoro baina ya familia ya Wayanga waliokuwa wa miliki wa eneo kabla ya kununuliwa na mwekezaji pamoja na wawekezaji wa eneo hilo.
“Kwenye vijiji kumekuwa na tabia moja mnapoitisha Mkutano watu wakaandika mahudhurio yao na kusaini inakuwa kama wamewapa kibali cha kwenda kufanya mnachotaka kufanya mnapokwenda kuandika mhitasari mwenyekiti na mtendaji mnaanza kuumba Mhitasari mwingine tofauti na yaliyojadiliwa kwenye mkutano hivyo achene kutumia majina na mahudhurio ya watu vibaya” alisema Mhe Batenga
Aidha amewaasa viongozi wa kijiji cha Ifumbo kutofautisha migogoro baina ya mtu mmoja na mwingine na migogoyo ya jamii na kijiji ili kuondoa taharuki katika jamii kwani hali hiyo inaweza kuzalisha migogoro mingine hivyo mgogoro wa mtu mmoja na mwingine isihusishe na jamii nzima iliyopo katika kijiji.
Akiongea kwenye kikao hicho kwa niaba ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chunya, katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya ndugu Msafiri Mayeye, amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kazi nzuri anayoifaanya ya kushughulikia changamoto mbalimali za wananchi na kumuomba aendelee kuwafuatilia wawekezaji hao mpaka watakapofikia hitimisho la mgogoro wao kwani Chama cha mapinduzi kinawakaribisha wawekezaji na hakitaki kuwapoteza wawekezaji hao
Naye Diwani wa kata ya Ifumbo Mhe.Weston Mpyila akatoa rai kwa watu wanaomiliki maeneo kuwa wakweli na wa wazi pindi wanapotaka kupangisha au kuuza maeneo yao ili kuzuia migogoro ambayo inaweza kujitokeza huku akiwaomba wakwekezaji ndugu Lukasi Mwamenza na ndugu Aidani Msigwa kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao lakini pia familia ya Wayanga waliokuwa wamiliki wa awali kuwa wakweli na kuweka kila kitu wazi wanapotaka kufanya jambo .
“Nitoe rai kwa watu wengine wenye maeneo wanapotaka kuyauza au kuyapangisha kuweka kila kitu wazi, lakini pia niombe hawa wawekezaji wawili msigwa na Luka waone namna wakae na kuumaliza mgogoo huu kwasababu wao ndio wenye kuumaliza ili wawe na Amani na mambo mengine yaweze kuendelea “alisema Mhe Mpyila
Kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa sita kwa lengo la kuumaliza mgogoro baina ya familia na wawekezaji kimehudhuriwa na kamati ya ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuanzia Ngazi ya wilaya , kata na tawi, watalamu mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Pamoja na Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali na viongozi wa kata na kijiji.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga akizungumza na wajumbe wa kikao wakati wa kusuluhisha mgogoro wa ardhi baina ya familia iliyokuwa ikimiliki eneo lililo nunuliwa na mwekezaji pamoja na wawekezaji hao katika kijiji cha Ifumbo
Katibu wa umoja wa Vijana kupitia chama cha Mapinduzi ndugu Msafiri Mayeye akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Chunya kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wakati wa kikao cha kusuluhisha mgogoro baina ya familia iliyokuwa ikimiliki eneo lenye mgogoro na wawekazaji kilichoketi katika kanisa la Pentekoste katika kijiji cha Ifumbo
Diwani wa kata ya Ifumbo Mhe Weston Mpyila akitoa rai kwa wananchi wa kijiji cha Ifumbo wanaomiliki maeneo kuwa wakweli na kuweka kila kitu wazi pale wanapotaka kuuza maeneo yao ili kuzuia migogoro inayoweza kujitokeza kutokana na udanganyifu
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.