KATIBU Tawala Mkoa wa Mbeya Bwa. Lodrick Mpogolo amewataka Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chunaya na taasisi za serikali kufuata Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Hayo ameyasema Leo November 2, 2022 katika kikao na watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri {Sapanjo Hall}.
Bwa. Mpogolo amesema kuwa Watumishi wa halmashauri na taasisi za serikali zilizopo wilaya ya Chunya waone umuhimu wa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kila mmoja awajibike katika nafasi yake.
“Kila Mtumishi hapa aone umuhimu wa kufuatilia na kuishi kwa kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa Umma”.
Aidha Bwa. Mpogolo alitoa rai kwa wataalamu kuhakikisha wanawajibika kwa nafasi zao ili kuleta maendeleo chanya ndani ya wilaya ya chunya
“Wataalamu katika nchi yeyote ndio injini ya maendeleo ya nchi ukitaka kuleta mabadiliko chanya ya wilaya ya chunya watu wa kwanza wa kuchochea maendeleo ni wataalamu na ndio maana ninyimpo hapa” amesema Bwa. Mpogolo
Kama wataalamu ilimuweze kufanya vizuri na kutimiza malengoyenu vizuri ni lazima muwe timu moja, ilituweze kuleta ufanisi katika halmashauri yetu ni kufanya kazi kama timu aliongeza kusema Bwa. Mpogolo.
Kwaupande mwingine Bwa. Mpogolo alisisitiza ukusanya wa mapato kwani bila ya mapato halmashauri haiwezi kujiendesha, ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato kiholela.
“Niwajibu wa kila mmoja kuhakikisha mapato yanaongezeka na sio kupungua kwa kuziba mianya ya kupoteza mapato” alisema Bwa. Mpogolo
Pia alisisitiza kuhakikisha aislimia 10 inapelekwa kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye walemavu, sambamba na kusimamia miradi yote inayotekelezwa na Halmashauri.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.