Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Lupa lililopo wilaya ya Chunya Wakili Athuman M Bamba amewatahadharisha wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata kutumia mitandao ya kijamii (WhatsApp) kuepuka kuchanganya wakati wa kutuma taarifa stahiki kwa tume au penginepo kwa mujibu wa miongozo na maelekezo waliyopewa na watakayoendelea kupewa kabla, wakati na baada ya Uchagzu mkuu unakaofanyika mapema Mwezi Oktoba 2025
Akizungumza wakati akitoa hotuba ya kuahirisha Mafunzo leo 6.8.2025 yaliyodumu kwa siku tatu katika ukumbi wa Mikutano wa Mwanginde Hall ulipo Jengo jipya la Utawala Wakili Bamba amewataka wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kuhakikisha wanapunguza matumizi wa ‘WhatsApp’ katika kipindi hiki wakati wanatekeleza Majukumu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
“Hivi sasa kuna makundi Sogozi (WhatsApp), Jitahidini katika kipindi hiki muyapunguze ili msije mkakosea kutuma taarifa ambazo hamkutakiwa kutuma huko” Amesema Wakili Bamba
Aidha Wakili Bamba ameendelea kuwasisitiza kwamba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi haikukosea kuwaamini kutekeleza majukumu ya tume katika maeneo yao ya uteuzi hivyo amewataka kuendelea kulinda Imani ya Tume kwao kwa kufanya kazi kwa haki na kwa weledi”
Mwenyekiti wa Mafunzo na Mshiriki wa Mafunzo hayo kwaniaba ya washiriki wengine Ndugu Obed Mwaikuka ametoa shukrani kwa Mkurugenzi mtendaji, pamoja na Tume huru ya Taifa kuwaamini kutekeleza Majukumu hayo muhimu, nyeti na yenye dhamana ya kupata viongozi watakao ongoza Taifa kipindi cha miaka mitano
Aidha Mwaikuka amemuhakikishia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Lupa kwamba vile walivyoaminiwa ndivyo watakavyotekeleza majukumu hayo kwa weledi na kwa kujituma huku akisema watafundisha na kutoa maelekezo hayo kwa wasimamizi wa vituo kama walivyoelekezwa wakati wa Mafunzo.
Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata katika Jimbo la Uchaguzi la Lupa yamedumu kwa siku tatu na yamehusisha washiriki arobaini (40) toka kata zote ishirini za Jimbo la Uchaguzi la Lupa. Mafunzo hayo ni miongoni mwa mambo mbalimbali yanayofanywa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unakuwa huru, wa Haki na usio na dosari yoyote
Washiriki wa Mafunzo wakiendelea na mjadala wakati wa Mafunzo kuelekea Uchagzu Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025
Washiriki wakifanya Mazoezi ya kutengeneza eneo salama la kupigia kura wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktaba 2025 wakati wa Mafunzo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.