Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona ameewaasa wasimamizi kuzingatia , kutekeleza na kusimamia Sheria, Kanuni na miongozo yote waliyofundishwa na kuelekezwa kwenye semina elekezi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaaa unaotaraji kufanyika Novemba 27, 2024.
Hayo ameyasema leo Septemba 30, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wa semina elekezi kwa wasimamizi wasaidiziwa uchaguzi wilaya ya Chunya ikiwa na lengo la kuhakikisha wanatekeleza jukumu la kusimamia Uchaguzi kwa Haki.
“Maelekezo haya yanayotolewa leo muyachukue na kuyabebe kwa uzito mkubwa kwa kwenda kuyatekeleza na kuyazingatia yote laliyoelekezwa na Msimamizi wa Uchaguzi kwani Uchaguzi wa serikali za mitaa ni maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu.” Alisema Kambona.
Afisa TAKUKURU wilaya ya Chunya ndugu Werenifrid Temba amewataka wasimamizi wa uchaguzi kutenda haki na kuto kujihusisha na masuala ya rushwa kwa kuzingatia maelekezo yoliyotolewa .
“Rushwa ni matumizi mabaya ya mamlaka ambayo umekabidhiwa kuyatekeleza, hivyo ni vizuri kufuata miongozo na taratibu pamoja na yale ambayo mmeelekezwa kwenda kuyafanya pasipo kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa maslahi binafsi” alisema Temba
Naye mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Wakali Athumani Bamba amewaongoza wasimamizi wa Uchaguzi kutafsiri Sheria, miongozo na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2024 huku akiwasisitiza mambo mbalimbali ikiwemo taratibu za upigaji kura , kuhesabu kura na kutangaza matokeo pamoja na mambo mengine mengi.
Semina hiyo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi imeenda sambamba nakuapishwa kwa wasimamizi wasaidizi hao ambapo Hakimu Mkazi Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe James Juliu Mhanusi amewaongoza kwenye viapo hivyo ili wakasimamie na kuyatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika semina hiyo kwa weledi mkubwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Afisa Takukuru Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Werenfrid Temba akiwafunza wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuto kujihusisha na masuala ya rushwa na kuwasisitiza kutenda haki kwa kutekeleza wajibu wao.
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wakiendelea kufuatilia semina elekezi juu ya mamba mbalimbali ya kutekeleza kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.