Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mbaraka Alhaji Batenga amewataka wananchi kujenga majengo bora ya kuishi ili kuendana na mabadiliko makubwa yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika wilaya ya Chunya miradi hiyo ni pamoja na umeme, Maji, Barabara yakutoka Tabora mpaka Mbeya likitolewa ufafanuzi na Batenga kuwa ujenzi huo upo kwenye mpango maalumu na kukamilika kwake kutaongeza mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi
Mhe Batenga ametoa kauli hiyo jana tarehe 28/2/2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kambikatoto ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake iliyodumu kwa siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Awali wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa nyakati tofauti walipopata nafasi ya kuzungumza namna idara na vitengo vyao vinavyosimamia miradi hiyo ya maendeleo katika mkutano huo wa mkuu wa wilaya na wananchi wa kambikatoto, wamekiri miradi hiyo inatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi wa nane kutokana na uhitaji wa miradi hiyo ukiwepo Mradi wa Maji pamoja na Umeme
Batenga akijibu maswali kuhusu uwepo wa migogoro midogo midogo kati ya wakulima na wafugaji amewataka wananchi kuwa watulivu kwani Serikali iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi jambo ambalo itaondoa kabisa changamoto ya migogoro ya ardhi wilani Chunya lakini pia ujenzi wa kituo cha Polisi cha Kambikato kitasaidia pia kupunguza Migogoro mbalimbali
Aidha Mhe Batenga amewataka viongozi wa kijiji kuandaa vikao na mikutano ya hadhara kwa lengo la kusoma mapato na matumizi kwa wananchi ili kusaidia kuondokana sitofahamu namna ya mwenendo wa kijiji husika, huku akisema ni haki ya wananchi kuhakikisha wanajua mapato na matumizi ya vijiji vyao
Ziara ya Mkuu wa wilaya ya Chunya ilianza tarehe 27/2/2024 na kuhimitishwa tarehe 28/2/2024 ambapo katika siku ya pili ya ziara miradi mbalimbai imetembelewa ikiwepo shule mbili za msingi ikiwa ni pamoja na shule ya msingi Kipembawe iliyojengwa kwa shilini milioni 538.5, kituo cha Polisi, Shule ya sekondari Kambikatoto na baadaye kufanya mkutano wa Hadhara kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu
Baadhi ya wananchi waliokuwa wanajitokeza kutoa kero kwa Mkuu wa wilaya,kusikiliza maelekezo ya serikali kwao juu ya mambo mbalimbali
Mkuu wa wilaya ya Chunya (Kulia mwenye Shati la Draft) akiongoza kamati ya Ulinzi na usalama kukagua miradi ya Maendeleo. Pichani ni mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kambikatoto
Mhandisi wa Halmashauru ya wilaya ya Chunya (Wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati alipoongoza kamati ya usalama ya wilaya ya kukagua miradi ya Maendeleo
Mkuu wa wilaya ya Chunya akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari Kambikatoto mapema jana wakati wa kuhitimisha ziara yake iliyodumu kwa siku mbili
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.