Wananchi wa kata ya Mafyeko wilayani Chunya wameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania fedha kiasi cha shilingi milioni 53 ili kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari ya kata hiyo ili kutatua changamoto watoto kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma ya Elimu, kwani awali walipaswa kusafiri umbali wa kilometa 40 kuifikia sekondari ya Isangawana
Akitoa taarifa mbele ya Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya Mwalimu Keneth Kaduma ambaye ni afisa Elimu kata ya Mafyeko na Katibu wa kamati ya Ujenzi wa Shule hiyo amesema mpaka sasa fedha shilingi milioni miamoja arobaini na moja, laki tano na elfu kumi na moja na mia sita (141,511,600) zimetumika ambapo halmashauri ya wilaya ya Chunya imechangia milioni 17, milioni 11 zilitolewa kwenye mfuko wa jimbo huku fedha nyingine ni michango ya wadau na wananchi wa kata ya Mafyeko
Mpaka sasa Madarasa mawili yamekamilika na yako tayari kwa matumizi huku zaidi ya dawati 70 yakiwa yamekamilika, madawati mengine 60 yako hatua za umaliziaji tayari kuletwa kwa matumizi, Madarasa mawili mengine yako hatua za jamvi. Ofisi ya walimu imekamilika sambamba na Ofisi ya Mkuu wa Shule zimekamilika
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye kiongozi wa ziara ya kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi Chunya Ndugu NOEL CHIWANGA amesema watawaagiza viongozi wa serikali wilayani Chunya kuaandaa andiko la kupeleka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuomba fedha za kukamilisha ujenzi wa shule hiyo
“Tunajua Rais na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan hawezi kushindwa kutuletea fedha za kukamilisha ujenzi wa shule yetu hii, Hivyo sisi kama chama tutawaagiza viongozi wa halmashauri waandike andiko la kuomba fedha za kukamilisha ujenzi hapa ili watoto wetu waanze kusoma hapa”
Aidha mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya amewapongeza wananchi wa kata ya Mafyeko kwa namna walivyojitoa kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo huku akisema huo ndio uzalendo kwa nchi yao, Amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya kuwasiliana na shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuona uwezekano wa kuhamisha nguzo za umeme mkubwa ambazo zimepita karibu kabisa na majengo ya shule akisema ni hatari sana kwa wanafunzi pale itakapotokea changamoto au hitilafu.
Miradi iliyotembelewa leo na kamati hiyo ni pamoja na Mradi wa Kituo cha Afya Kambikatoto ambapo Jengo la wagonjwa wa Nje (OPD), Maaabara, jengo la upasuazi na wazazi, jengo la kufulia pamoja na Nyumba ya kuishi watumishi, Mradi wa Barabara kutoka Kambikatoto kwenda Sipa, Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya walimu(3 in 1) shule ya msingi Sipa yenye uwezo wa kubeba familia tatu za watumishi, Mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Bitimanyanga, Mradi wa Kituo cha Afya Mafyeko, na Shule ya Sekondari Mafyeko
Katika Miradi iliyotembelewa na kamati ya siasa ya Chama pamoja na shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za kujenga miradi mbalimbali pia kamati hiyo imeshauri wataalamu kuhakikisha changamoto ndogo ndogo kwenye miradi hiyo zinatatuliwa haraka ili kuletaufanisi katika miradi hiyo
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya Chini ya mwenyekiti wake Ndugu Noel Chiwanga iko katika Ziara ya kawaida katika kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo kama ilani ya Uchaguzi ya Mwka 2020-2025 inavyoelekeza.
Jengo lenye Vyumba viwili vya Madarasa vilivyokamilika Shule ya Sekondari Mafyeko
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.