Wananchi wa Kata ya Matwiga Wilaya ya Chunya jana wameungana kuadhimisha siku ya mazingira Duniani inayofanyika Juni 5 kila mwaka
Madhumuni ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo mazingira, aidha kuhamasisha jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuifadhi na kulinda mazingira.
Wananchi wa Kata ya Matwiga wameadhimisha maadhimisho hayo ya siku ya mazingia kwa kwenda kufanya usafi katika maeneo mbalimbali dhumuni likiwa ni kuhakikisha mazingira yao yanakuwa safi na salama.
Shughuli mbalimbali zinazohamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali zimefanyika zikiwemo
ufyekaji wa maeneo yanayozunguka mradi wa bwawa la maji kata ya Matwiga kijiji cha Matwiga, kufanya usafi katika shamba la miti la AMCOS Matwiga, pia kufanya usafi kwenye shamba la miti la Ndg Bupe Semen.
Kaulimbiu ya kimataifa inayoongoza maadhimisho haya ni “Air Pollution” {Uchafuzi wa Hewa} ambapo kimataifa maadhimisho haya yatafanyika nchini China.
Pamoja na kaulimbiu ya kimataifa, kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira mwaka huu kitaifa ni “Tumia mifuko mbadala ya plastiki; kwa ustawi wa Afya, Mazingira na Maendeleo ya Uchumi”.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.