Wananchi wa kata ya Kambikatoto wilayani Chunya wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia fedha kiasi cha shilingi milioni 583,180,028 ili kujenga shule ya sekondari katika kata hiyo ambayo pamoja na ukubwa wa kijiografia wa kata hiyo hata umbali kutoka kata hiyo mpaka kata nyingine ilikuwa bado haina shule ya sekondari ya kata.
Wakizungumza mbele ya kamati ya fedha, uongozi na mipango ya baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati kamati hiyo ilipopita kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wananchi wamesema serikali ina wajali sana kwani si muda mrefu kituo cha afya kambikatoto kimejengwa na sasa shule ya sekondari inajengwa.
“Tunashukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan kutujengea Shule ya Sekondari yenye vyumba karibu kumi na mbili (12) kwenye Kata yetu jambo ambalo mimi sikuwahi kufikiria, Mimi nilijua tutaanza na madarasa mawili au matatu hivi, lakini serikali kwa wakati mmoja vyumba vya madarasa karibu 12 kwakweli tunaishukuru sana serikali. Alisema Ndugu Mwita Chacha.
“Mweshimiwa mwenyekiti wa Halmashauri sisi tunakushukuru wewe na kamati yako kuja kututembelea ili kukagua mradi huu lakini pia tunaishukuru sana serikali kutuletea mradi huu lakini pamoja na hayo tunaomba utusaidie kutazama upya bei za milango na fremu zake bei iliyowekwa ni sawa na bei za mjini wakati huku sisi bei za mbao zina nafuu kuliko mjini pia wananchi wengi huko mtaani wanamashaka na eneo hili eneo la bei za milango na fremu zake” Alisema Mathias Aloice Songo.
Naye Blandina Chingwile alisme “Mwenyekiti pamoja na kamati yako tunakushukuru kuja kutembelea mradi huu na kipekee sana tunaishukuru serikali kwa kutupatia mradi huu, Tulifanikiwa katika ujenzi wa kituo cha afya hatuwezi kushindwa kusimamia ujenzi wa shule hii hivyo mwenyekiti wewe uwe na amani kabisa. Pia usisite kuja au hata kupiga simu pale unaposikia changamoto maana lengo la serikali ni kutusaidia kutatua kero kwa wananchi wake”.
Kamati ya fedha, uongozi na Mipango (FUM) imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule hiyo kwani ni yao na itawasaidia wao wenyewe na familia zao na kwakufanya hivyo watakuwa wametekeleza na kuulinda utaifa na uzalendo wao kwani serikali inapowaletea fedha haina maana wananchi hawatakiwi kushiriki kabisa.
Aidha kamati hiyo kupitia mwenyeki wake Mhe Bosco S Mwanginde imewaagiza viongozi wanaosimamia mradi huo kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha inayotokana na nguvu za wananchi wa kata hiyo na baada ya kupata taarifa hiyo kamati hiyo itafanya ziara tena ili kuzungumza na wananchi maana serikali ya awamu ya sita inataka uwazi na ushirikshwaji wa jamii kuwa kipaumbele cha kwanza.
Kaimu afisa Elimu sekondari Mw. Nikusuma Kamoma amewataka wananchi kusimamia vizuri matumizi ya pesa hizo jambo ambalo kwanza litawapa sifa njema na nzuri lakini pia pesa zitakazo baki zinaweza kuanza mradi mwingine katika kata hiyo jambo ambalo litafanya kata hiyo kuwa na kasi katika maendeleo lakini kinyume chake mtaichafua wilaya ya Chunya jambo litakalosababisha wilaya ikakosa uaminifu na kupelekea serikali kusita kuleta pesa sababu tu usimamizi mbaya.
Kata ya Kambi katoto ina jumla ya wanafunzi 298 wanaosma elimu ya Sekondari madarasa tofauti tofauti nje ya kata hiyo ambapo shule iliyo karibu kwa sasa ni umbali wa zaidi ya kilometa 40 ina kidato cha kwanza pekee wakati shule nyingine iko umbali wa kilometa 80 kutoka kambikatoto hivyo ujenzi wa shule hiyo ni ukombozi wa kielimu wa wananchi wa kata ya Kambikatoto kwa ujumla.
Mafundi wako eneo la kazi wakiendelea na shughuli za kupaua majemngo mbalimbali shule ya sekondari Kambikatoto
Wanaonekana wakitembea karibu na jengo hilo ni wajumbe wa kamati Fedha, Uongozi na Mipango wakitembelea Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Kambikatoto
Baadhi ya Majengo yanayojengwa Kambikatoto kwaajili ya Shule Mpya ya sekondari Kambikatoto inayotaraji kuanza kuchukua wanafunzi mwaka 2024
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.