Maafisa Elimu kata, watendajiwa kata na vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wametakiwa kuwafuatilia na kujua walipo wanafunzi wote wa kidato cha kwanza hambao bado hawajaripoti shuleni hadi sasa.
Haya yame semwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka leo tarehe18, January 2023 kwenye ziara yake iliyolenga kukagua na kuona hali halisi ya kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ndani ya wilaya.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya amewaelekeza Maafisa elimu kata, watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha watoto wote ambao bado hawajaripoti shuleni mpaka sasa wanatafutwa popote walipo na kuripoti katika shule walizo pangiwa.
Mayeka amesema hali ya watoto kuripoti shuleni sio ya kuridhisha sana kwani idadi kubwa ya wanafunzi bado hawajaripoti shuleni
Aidha Mhe. Mayeka amesema hakubaliani kabisa na sababu zinazotolewa na wazazi za kutokufanya maandalizi ya sare na vifaa mbalimbali vya shule, hivyo kupelekea kuchelewa kwa watoto kuripoti shuleni kwani walipaswa kufanya maandalizi hayo mapema.
“Hii haikuwa ni dharura, kwamba shule zilikuwa zinajulikana zinafunguliwa lini hivyo mzazi alipaswa kufanya maandalizi mapema” alisemaMayeka
Hata hivyo Mhe Mayeka amesema hivi karibuni wataanza zoezi la kupita nyumba hadi nyumba kuwasaka watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na mpaka sasa bado hawajaripoti shuleni na kuwachukulia hatua wazazi wote ambao hawajawapeleka watoto shuleni.
“Tayari tumeshaandaa migambo kwa ajili ya kuzunguka nyumba hadi nyumba kukamata wazazi wote ambao hawajatekeleza wajibu wao wa kuwapeleka watoto Shuleni” amesema Mayeka.
Hatuwezi kukubali jambo hili tunaenda kuchukua hatu, hatuta muonea huruma mzazi yeyote, ilipasiwepo na usumbufu wa aina yeyote tunaomba watoto wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wafike shule
Mkuu wa wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Ujenzi wa vyumba vya madarasa, halmashauri ya wilaya ya chunya haina upungufu wa vyumba vya madarasa.
Kwaupanda wa Afisa Elimu Sekondari wa halmashauri ya wilaya ya chunya Ndugu Hamis Mapoto amesema wilaya ya chunya wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 ni wanafunzi 3885 na mpaka kufikia jana tarehe 17, ni wanafunzi 1653 wamesha repoti sawa na asilimia 42.5/%.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama na Wataalamu wa Halmashauri wamekagua Shule za sekondari Itewe, Isenyela, Kipoka, Makongolosi pamoja na shule ya sekondari Makalla.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe, Mayeka S Mayeka wakwanza kushoto akiwa sambamba na Afisa Elimu Sekondari wa halmashauri ya wilaya ya chunya kwenye ziara ya kuona hali halisi ya kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ndani ya wilaya.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S. Mayeka akifuatilia taarifa ya kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika moja ya shule alizo zitembelea
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.