Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeandika rekodi ambayo haijawahi kuwepo katika Historia ya uwepo wa Shule za upili (A Level) kwa kufaulisha wanafunzi wote waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka huu 2024 katika mitihani iliyofanyika mapema mwezi May 2024 ambapo wanafunzi 643 wamefaulu kwa daraja la kwanza na daraja la pili huku wanafunzi nane tu wakifaulu kwa daraja la tatu
Juhudi inayo oneshwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ujenzi wa miundombinu ya Shule katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeendelea kuzaa matunda kwa wanafunzi wote wa Shule ya Sekondari Kiwanja na Shule ya Sekondari Lupa kufaulu kwa Daraja la kwanza , Daraja la pili na Daraja la tatu tu
Kwa matokeo hayo ni dhahiri kwamba viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Chunya wanapata huduma bora na nzuri katika Nyanja zote ikiwepo Elimu
Ikumbukwe Halmashauri ya wilaya ya Chunya ina shule Mbili tu za Upili (A Level) ambayo ni hule ya Sekondari Kiwanja na Shule ya Sekondari Lupa lakini Halmashauri iko mbioni kuongeza Shule mbili za upili ambazo ni Shule ya Sekondari Sangambi na Shule ya Sekondari Makongolosi
Mchanganuo wa Matokeo ni kwamba Shule ye Sonkdanri Kiwanja ina Daraja la kwanza 269, Daraja la pili 79 na daraja la tatu 4 wakati Shule ya Sekondari Lupa ina daraja la kwanza 190, daraja la pili 106 na daraja la tau ni 04. Katika Shule zote hakuna daraja la nne na daraja sifuli
Kwa undani wa matokeo bonyeza kiunganishi hapo chini
KIWANJA SEKONDARI https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/acsee/results/s1584.htm
LUPA SEKONDARI https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/acsee/results/s0774.htm
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.