Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera amewataka wakuu wa idara mbalimbali wilayani Chunya Kushirikiana na Mtunza hazina (DT) wa halmashauri kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ili kurahisisha kupata taarifa sahihi ambazo zinapelekea kufutika kwa hoja hizo
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya lililoketi jana tarehe 14/6/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) lenye lengo la kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali zilizoibuliwa katika ukaguzi kwa Mwaka wa fedha 2021/2022
“Hoja hizi za CAG wengi wanafikiri Mtunza hazina (DT)ndo anahusika kupambana na hojo hizi, Lazima wakuu wa idara wote tuhusike kuzijibu, Mkurugenzi unda timu maalumu ya kushugulikia hizi hoja. Ndo hoja za mkaguzi wa ndani lazima zishughulikiwe kwani ndizo zinageuka kuwa hoja za CAG hivyo zishughulikiwe mapema. Na wewe mkaguzi wandani hoja zako ukishazibua mwandikie mkurugenzi na nakala aipate mkuu wa wilaya ili naye ajue kwamba kuna hoja na hii ifanyike kwa mkoa mzima
Aidha Mhe Homera amewapongeza viongozi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwakuendelea kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kupelekea halmashauri ya wilaya ya Chunya kuongoza katika Mkoa wa Mbeya kwa kukusanya zaidi ya asilimia 109 zaidi ya lengo lililokusudiwa awali
Niwapongeze kwa kukusanya mapato mengi, kwakweli mmetutoa kimasomaso kwani mlitakiwa kukusanya Bilioni 5.3 lakini sasa mmekusanya Bilioni 5.9 sawa na asilimia 109 hongereni sana. Na bila shaka timu yenu iko vizuri na muendelee kushirikiana hivyo ili muendelee kututoa kimasomaso
Katibu tawala mkoa wa Mbeya Ndugu Rodrick Mpogolo amewapongeza viongozi wote wa halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa namna wanavyosimamia miradi ya maendeleo jambo lililopelekea halmashauri ya wilaya ya Chunya Kupata Hati safi, huku akiwata kuendelea kujenga umoja na mshikamano kati ya baraza la madiwani na watumishi wengine wa halmashauri ili muendelee kupata hata safi kwa wakati mwingine
Niwapongeze viongozi wote na Manejimenti kwa kazi nzuri wanayoifanya ndo maana wakaweza kupata hati safi, lakini ni imani yangu kwamba Mwenyekiti wa Halmashauri mtaendelea kujenga ushirikianao kati ya baraza la madiwani na viongozi wengine wakiwepo watumishi ili wakati mwingine mpate hati safi nyingine
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S. Mayeka amemuhakikishia mkuu wa Mkoa mambo yote aliyoshauri kwaajili ya maendeleo ya wilaya ya Chunya yatatekelezwa kama alivyoshauri, pia amewashukuru madiwani, wakuu wa idara na watumishi wengine kwa kazi kubwa wanayoifanya katika suala zima la makusanyo ya mapato
Tutajitahidi kutekeleza maagizo na ushauri wako kama ulivyotuagiza, lakinin pia nimwapongeze madiwani, wakuu wa idara na watumishi wote kwa kazi kubwa wanayofanya katika suala la ukusanyaji wa mapato, Natambua kazi kubwa ambayo watumishi wanafanya na naomba tuendelee kupamabana ili tuendelee kuwa vinara kataka suala la ukasnayaji wa mapato
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amesema Chunya tutaendelea kushirkiana vizuri ili kuhakikisha tunaendelea kutekeleza miradi yote ya maendeleo kwa ufasaha na baraza hili liko tayari kuendeleza ushirikiano huo ili tuendelee kuwa vinara katika makusanyo ya mapato na hata utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Chunya
“Mimi siwezi kuanza kurudia mambo ambayo viongozi wengine wameshayazungumza, sisi tuko tayari kutoa ushirikiano unaohitajika ili tuweze kufunga hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za serikali.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.