Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Stephen Nindi amefanya mkutano wahadhara na wakulima wa Wilaya ya Chunya Oktoba 4, 2025 kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima kutokana na kilimo kuwa ni sayansi inayohitaji matumizi sahihi ya mbolea yenye vipimo sahihi kulingana na afya ya udongo.
Awali akiwa katika kikao na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dkt. Nindi amepongeza juhudi za viongozi wa Wilaya ya Chunya kwa kupata mashine za kupimia afya ya udongo ili kumrahisishia mkulima kutambua aina ya udongo na mbolea inayopaswa kutumika.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Chunya SACI Mbaraka Batenga amesema, upimaji wa afya ya udongo ni muhimu kwakuwa unamwezesha mkulima kutumia mbolea kwa usahihi na kuongeza uzalishaji wa mazao.
“Msimu wa Kilimo ulioisha mwaka 2024/2025, zao la Tumbaku limefanya vizuri, mbolea iliyosambazwa na Kampuni ya Mbolea Tanzania - TFC imeongeza uzalishaji zaidi ya makadirio yaliyokuwepo ambapo Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya imezalisha tani milion 27,091.7 na kuondoa malalamiko kwa wakulima,” ameeleza SACI Batenga.
Pamoja na mafanikio hayo ameeleza kuwa bado yapo maeneo ambayo hayana mwamko wa kutumia mbolea kama eneo la kata ya Kambi Katoto na Sipa hivyo endapo watapewa elimu ya matumizi ya mbolea watahamasika kutumia mbolea na kuongeza uzalishaji.
Dkt. Nindi amefanya Mikutano miwili ya hadhara, mmoja katika kata ya Lupa, tarafa ya Kipembawe na mkutano mwingine ameufanya Itumba, tarafa ya Kiwanja huku akipongeza juhudi za wakulima kuongoza kuzalisha mazao kutokana na matumizi sahihi ya mbolea.
Kuhusu usambazaji wa mbolea, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania - TFC, Bw. Samuel Mshote ameeleza kuwa katika msimu wa Kilimo uliopita TFC ilisambaza tani 61,000 ya mbolea ya NPK 10:18:24 kwa wakulima wa zao la Tumbaku. Ameongeza kwa mwaka huu, TFC imepanga kusambaza takribani tani 71,000 za mbolea ya NPK 10:18:24 ambapo usambazaji wa mbolea ya NPK 10:1824 kwa Wilaya ya Chunya umefikia asilimia 85, tani 10,395 zimewafikia wakulima kati ya tani 12,230 zinazotarajiwa kusambazwa katika msimu huu.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Stephen Nindi na wajumbe wake
wakati wa kikao cha ndani leo Oktoba 4,2025 katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dk. Stephen Nindi akifuatilia kwa karibu kikao cha ndani na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Batenga.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.