Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewataka watumishi wa serikali hasa vijana kuwahudumia wananchi wa Tanzania wanaoishi wilayani Chunya Kizalendo maana wana umri mrefu zaidi wa kufanya kazi kuitumikia serikali na wananchi wake kwa ujumla
Mhe Mayeka ametoa kauli hiyo leo tarehe 11/8/2023 alipokuwa akizungumza na wahudumu wa afya wa kituo cha Afya Mafyeko wakati alipoiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Chunya kukagua miradi Mbalimbali itakayopitiwa na Mwenge wa uhuru unaotarajiwa kukimbizwa wilayani Chunya mapema mwezi Septemba 13 na 14 mwaka huu 2023 huku miradi mbalimbali ikiwepo miradi ya Elimu, Afya, Maji na miradi mingine kupitiwa na mwenge huo
“Fanyeni kazi kwa bidii kuwahudumia wananchi ukizingatia umri wenu bado ni mdogo hivyo mnayo nafasi ya kufanyakazi muda mrefu sana hivyo jitumeni sana kuweni na moyo wa uzalendo kuwahudumia wananchi wa Tanzania wanaoishi wilayani Chunya”
Aidha Mhe Mayeka amewataka watumishi kutoka Makao makuu kuhakikisha miradi inayotekelezwa wilayani Chunya inatekelezwa kwa kiwango sahihi na iendane na thamani ya fedha inayotolewa kinyume na hapo maana yake hatutekelezi majuku yetu ipasavyo.
Awali akitoa taarifa za kituo hicho Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mafyeko Dkt Samwel Macha. Amesema kituo hicho kina wahuduma watatu wote wakiwa chini ya miaka mitano tangu kuajiriwa lakini na kituo kinahudumia zaidi ya wananchi 400 mpaka 500 kwa mwezi mmoja hivyo azma ya serikali kuwasogezea huduma wananchi imefanikiwa sana
“Kwa mwezi mmoja kituo kiahudumia wagonjwa wan je mia nne mpaka mia tano (400-500) na wakina mama wanaokuja kufungua kadi (Wajawazito) ni wastani wa sitini (60) kwa mwezi na wakati wakinamama wanaokuja kujifungua ni wastani wa wakina mama arobaini mpaka arobaini na tano “40-45” kwa kwezi
Ziara ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Chunya imedumu kwa siku moja na imekagua mradi wa shule ya awali na msingi ya mchepuo wa kiingereza, mradi wa Maji Matundasi, mradi wa zahanati ya Igangwe, kituo cha Afya Mafyeko pamoja na eneo ambalo kutafanyika mkesha wa Mwenge uwanja wa mpira wa Miguu biti Manyanga
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka akiingia kwenye moja ya vyumba vya kutolea huduma katika kituo cha Afya cha Mafyeko wakati alipoongoza kamati ya ulinzi na usalama kukagua miradi ya maendeleo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka akisoma orodha ya dawa zilizoletwa katika kituo cha Afya Mafyeko kwaajili ya kuwahudumia wananchi wanaohudumiwa na kituo hicho
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mafyeko Daktari Samweli Macha(Mwenye shati jeupe) akifafanua jambo mbele ya kamati ya ulizni na usalama ilipotembelea kituo hicho leo
Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Chunya Ikikagua mradi wa maji Matundasi
Kamati ya ulinzi na usalama ikishirikiana na baadhi ya watalam kutoka halmashauri ya wilaya ya Chunya wakikagua uwanja utakaotumika kwaajili ya mkesha wa Mwenge wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka (anayezungumza) akitoa mapendekezo ya marekebisho baadhi ya maeneo kwenye uwanja utakaotumika kwaajili ya mkesha wa mwenge mwaka huu 2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.