Mkuu wa wilaya ya chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amewataka wamiliki wa Leseni za uchimbaji wanaoendesha shughuli zao katika hifadhi ya Msitu wa mbiwe wilayani chunya kuorodhesha wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika machimbo yao, ili kwa ambao hawapo sehemu yoyote kuondoka kwenye msitu huo.
Mhe. Mayeka ametoa agizo hilo jana June 13, 2023 akiwa kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wanaofanya kazi katika machimbo hayo ambako alienda na kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya na maafisa mbalimbali wa Taasisi za Umma kwa ajili ya kuona uvamizi na uharibifu mkubwa unaoendelea katika hifadhi ya msitu wa mbiwe.
“Hawa wamiliki watawaandika watu wanaofanya kazi kwenye machimbo yao na watu wasiokuwa na machimbo tutawaomba waondoke kwenye msitu huu waende sehemu nyingine wakafanye shughuli zao” alisema Mhe. Mayeka
Mhe. Mayeka amewataka wamiliki wa leseni za uchimbaji katika msitu huo kuhakikisha wafanyakazi wao wanakuwa na vitambulisho vitakavyo wawezesha kuingia katika msitu wa mbiwe na kuendelea na shughuli za uchimbaji
“Kuanzia leo watu wenu wawe na vitambulisho na hivyo vitambulisho kopi moja unabakia nayo wewe na nyingine TFS, ili tukiingia humu asiyekuwa na kitambulisho ndio tunaye mtaka” aliongeza kusema Mhe. Mayeka
Alisema Najua kuna watu hawapo kwenye zamu (shift) ya mtu yeyote hapa wanazunguka usiku na mchana na ndio wanavamia leseni za watu wanaanza kuchimba na wakikutwa wanakimbia na ndio wanaotuharibia Msitu.
Diwani mwenyeji wa kata ya matundasi Mhe. Kimo Choga amesema wanatambua kuwa wapo kwenye eneo la hifadhi ya msitu ila kilicho wapeleka huko ni kutafuta ridhiki ya maisha yao.
“Nahapa tulipo kuna watu ambao wanafanya biashara ndogondogo kama mamantilie na vilevile kuna watu mbao wanafanya kazi za uchimbaji kwenye leseni zilizopo hapa ambazo nazitambua kama leseni mbili” alisema mhe. Kimo
Mhe. Kimo aliongeza kuwa "Mheshimiwa mkuu wa wilaya tunafahamu kabisa tupo hapa hatupo kisheria hivyo naomba nikiri kabisa mimi na wananchi wangu, lakini matumaini yetu sisi ni kupokea maelekezo ya namna ya kuishi kisheria kwenye eneo hili la hifadhi ya msitu".
“Kwa niaba ya wananchi mimi na kuahidi kwamba kama kunanamna yeyote yakupata maelekezo ya kuishi kisheria kwenye eneo hili sio kwa kujenga makazi ya kudumu nikufanya biashara ya muda mfupi na ndio maana makazi yetu sio ya kudumu” amesem Mhe. Kimo
Wachimbaji wadogo wanaofanya shughuli za uchimbaji kwenye Msitu wa Mbiwe wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S Mayeka kwenye mkutano wa Hadhara
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.