Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Homera ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kusimamia kikamilifu na kufanikisha Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa inayotekelezwa kupitia Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Mh. Homera ametoa pongezi hizo katika Hafla ya Uzinduzi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Lupa kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kukamilisha Ujenzi wa vyumba 110 kwa asilimia 100, Ikiwa sambamba na Ukamilishaji wa Madawati pamoja na viti.
"Mimi nimefarijika sana nimeyaona madarasa yamependeza na nikiritu kwamba nimeyapokea yote 110 Ahsanteni sana" Mh Homera Mkuu wa mkoa wa Mbeya
Pia alisema Wanafunzi 3288 waliopangiwa kujiunga na kitado cha kwanza katika wilaya ya chunya watakaa kwenye madawati na madarasa yaliyokamilika, sambamba na hilo halmashauri ya wilaya ya chunya inayo ziada ya madarasa 21.
“Geografia ya wilaya ya chunya tunaifahamu mazingira yake ni magumu lakini pamoja na changamoto hizo nikupongeze Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wafanyakazi wote kwani mmefanikisha kuijenga miradi hii kwa kiwango cha hali ya juu sana ahsanteni”. Mh Homera
Niwapongeze pia wananchi wa halmashauri ya wilaya ya chunya kwa Ushirikiano mkubwa walio onyesha wakati wa kujenga madarasa haya na kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bw Tamim Kambona akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Juma Homera wakati wa Hafla ya kukabidhi miradi hiyo, alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya chunya ilipokea Shilingi 2,600,000,000.00 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba 110 vya Madarasa katika Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari ambapo Ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 100 ilikwa ni pamoja na utengenezaji wa Madawati 2360.
Mkurugenzi Kambona alieleza kuwa kwa sekta ya Elimu Sekondari Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 900,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 45 vya madarasa katika shule 12 za sekondari pamoja na utengenezaji wa viti na meza, ambapo kwa sekta ya Elimu Msingi Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 1,300,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 65 vya madarasa katika vituo shikizi 20 ikiwa sambamba na utengenezaji wa meza na madawati.
Pichani:Mkuu wa Mbeya Mh Juma Homera akizundua moja kati ya vyumba 110 vya Madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Lupa Mradi ambao umekamilika
Muonekano wa Vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Lupa wakati wa Uzinduzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bw Tamim Kambona akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya UVIKO 19 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Juma Homera Januari 14, 2022
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.