Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Ismail Ally Ussi amefurahishwa na mradi wa zahanati ya Everest unaotokana na mkopo wa asilimia 10% uliotekelezwa na vijana watano kwani mradi huo umeiheshimisha Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kuwa umelenga maono ya serikali na ni mradi wenye tija kwa jamii na vijana hao.
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Ismail Ally Ussi Leo tarehe 7/10/2025 wakati akizindua mradi huo uliopo kata ta Matundasi Wilaya ya Chunya.
“Miongoni mwa vijana ambao wataweka historia leo katika taifa hili ni pamoja na vijana hawa watano walionufaika na mkopo wa asilimia 4% inayotolewa kwa vijana kupitia mkopo wa asilimia 10% kwani wameiheshimisha Chunya kwakuonyesha uzalendo ,ukamavu na uahodari katika kutimiza maono ya serikali ya kuwainua vijana” amesema Usssi
Vijana hawa wametupa heshima kubwa kupitia mwenge wa uhuru kwa kazi kubwa waliyoifanya kwasababu wanatambua leo hii miongoni mwa mambo ambayo rais Samia Suluhu Hassan anayafanya ni kuendelea kuibua fursa mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto katika jamiiwa ikiwa ni pamoja na vijana.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaj batenga amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa watu wote wanaokidhi vigezo na kufuata taratibu huku kipaumbele ikiwa ni kwenye miradi inayo lenga kuajiri na watu wengine ili kutatua changamoto ya ajira lakini pia kuinua uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Nikuhakikishie kiongozi kwenye Halmashauri yetu bado pesa zipo , tuna million mia nane tunasubiri watu wengine wakamilishe utaratibu tuwape pesa hizo kipaumbele ikiwa ni kwenye miradi inayozalisha ajira kwa watu wengini, mikopo ipo tunatoa kwa wazi kwa watu wote “ alisema mhe. Batenga
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo katibu wa kikundi hicho ndugu Goodanswer Ntogole amesema kuwa lengo la kuanzisha mradi huo ni kwaajili ya kujiajiri wao wenyewe kwaajili ya kujipatia kipato pamoja na kuisaidia jamii inayowazunguka kwa kutoa huduma mbalimbali za kitabibu pamoja na kutoa ajira kwa watu wengine.
Mkopo wa asilimia 10% unaolenga wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu unatolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwaajili ya kuwainua na kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi ikiwa ni adhima ya serikari katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Ismail Ally Ussi wakati wa kuzindua zahanati hiyo iliyojengwa kupitia mkopo wa asilimia 10
Katibu wa kikundi cha Upendo (Everest ) akisoma taarifa ya mradi wa Zahanati ya Everest iliyoko Matundasi wakati wa kuzinduliwa mradi huo na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Ismail Ally Ussi.
Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa ndugu Ismail Allly Ussi akipokea maelezo kuhusu makundi ya vyakula alipotembelea banda la lishe wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Everst katika kata ya Matundasi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.