UZINDUZI WA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYA YA CHUNYA.
Siku ya tarehe 15/11/2017 ilikua ni siku maalum ya uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika wilaya ya chunya, ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni mkuu wa wilaya ya chunya Bi. Rehema Madusa akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa H/w chunya Bi Sophia Kumbuli, mbali na uzinduzi wa jukwaa hilo pia kulikua na uzinduzi wa Tovuti ya Saccos ya wilaya Pamoja na uchaguzi wa viongozi wa jukwaa la akinamama wilaya ambapo Mwenyekiti wa jukwaa la akinamama wilaya aliyechaguliwa ni Bi. Esther Mpanja na katibu wake ni Bi salome Donatus. Mkurugenzi Mtendaji pia alipata fursa ya kuongea na akina mama na kuwatangazia kuwa Halmashauri ipo pamoja nao na kwamba zaidi ya Tsh. Mil 100 zimetengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuwakopesha akina mama na vijana.
Pia katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Saccos wa wilaya alitangaza kuwa wana mtaji wa jumla ya Tsh. Bil 3.4 ambapo mkuu wa wilaya aliwashauri kuwa wanaweza kufungua Benki yao na kuweza kukopeshana wao kwa wao pamoja na wananchi kwa riba ndogo.
Shughuli hiyo iliratibiwa na Idara ya Maendeleo ya jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Mgeni Rasmi wa katika uzinduzi wa Jukwaa la wanawake Chunya Mkuu wa Wilaya ya Mh.Rehema Madusa(mwenye kilemba chekundu) akiingia ukumbini, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa H/W Chunya Bi. Sophia Kumbuli
Mkurugenzi Mtendaji wa H/W Chunya Bi. Sophia Kumbuli akiongea na Jukwaa la Wanawake, kushoto kwake ni mratibu wa shughuli hiyo Ndg. David Ngowo
Afisa Maendeleo ya Jamii (w) Bi.Esther Mwakalile (katikati) akiongea na Jukwaa la Wanawake,
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.