Leo tarehe 26/6/2018 kimefanyika kikao cha uwindishaji wa kitalii cha kila mwaka kilichofunguliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya chunya
Mh. Rehema Madusa ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Sapanjo, Makao makuu ya Halmashauri ya Chunya.
Katika salamu zake kwa wadau, wataalam, na watu wote waliohudhuria Mh. Mkuu wa wilaya alianza kwa kumshukuru Mungu
kwa kuwawezesha watu wote waliohudhuria kufika salama ili kuweza kujadili kwa pamoja masuala yote yanayohusu uwindishaji na uhifadhi.
aligusia umuhimu wa uhifadhi kwa kusema na ninanukuu “huwezi kufanya uwindishaji au uwindaji kama hakuna uhifadhi, na pia bila
kusimamia utunzaji mazingira ipasavyo huwezi kufanya uwindishaji na kuwa na wanyama wa kutosha ambao watasaidia
kufanikisha uwindaji endelevu, pamoja na maendelo kwa wananchi wanaozunguka hifadhi na serikali kwa ujumla”. Mh. Mkuu wa
wilaya aliwashukuru wadau walioshiriki katika Operesheni za kuwaondoa wavamizi katika maeneo ya hifadhi kwani lengo
lilikuwa ni zuri ikiwemo kurejesha uoto wa asili, kusimamia sheria ili kuweza kuwadhibiti wale wote wanaokwenda kinyume cha
sheria na taratibu za nchi. Alisistiza wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka hifadhi wanahitaji Elimu, kusimamiwa na
wanahitaji viongozi wenye dhamira na nia ya dhati katika kusimamia sheria na taratibu za nchi kuhakikisha kwamba maeneo
yaliyohifadhiwa yanasimamiwa kisheria na wanaofanya uhalifu wanachukuliwa hatua za kisheria. Aliendelea kusistiza kuwa
kunauharibifu mkubwa sana wa mazingira kama vile vyanzo vya maji, akitolea mfano eneo la Mafyeko kuna sehemu/eneo
muhimu sana la chanzo cha mto lupa; pia maeneo ya Bitimanyanga kata ya mafyeko na kambikatoto kunafanyika ujangilli wa
hali ya juu kabisa na majangili hao wanajifanya wakulima na wafugaji kwani wakati ilipofanyika operesheni zilikamatwa
silaha za moto. Kwahiyo watu hao ni wahalifu na kwa pamoja ziunganishwe nguvu ili kuweza kuwadhibiti.
Naye Afisa Wanyamapori wilaya ya Chunya alipata fursa ya kuwasilisha taarifa ya idara ya maliasili ambapo pamoja na mambo
mengine alieleza vitalu vinavyopatikana katika wilaya ya chunya ni Rungwa South open area, Rungwa Mzombe Open area, Piti
west(Open area) GR, piti East Open area, Chunya Lukwat(open area) GR, sehemu ya eneo la kitalu cha Rungwa Inyonga GR, na
vitalu vinavyopatikana katika wilaya ya Songwe ni pamoja na Chunya Msami (open area) GR, Lukwati north GR, Lukwat South
GR, na Chunya East open Area; hii ni kifuatia mgawanyo wa wilaya ya Chunya ambapo wilaya mpya ya Songwe ilizaliwa. pia
aligusia juu ya mgawanyo wa fedha za asilimia 25 za uwindishaji wa kitalii unaotoka serikali kuu. fedha hizo ni mapato ya
uwindishaji yatokanayo na malipo ya wanyapori waliowindwa kisheria katika maeneo ya vitalu husika, aliongeza kuwa mgeni
hulipia fedha wizarani na baada ya malipo hayo kanuni za uwindishaji kitalii zinaitaka wizara kurudisha asilimia 25 kwenye
maeneo ya vijiji ama wilaya walipowindwa wanyama hao na katika fedha hizo asilimia 60 hupewa vijiji vinavyozunguka maeneo ya vitalu
husika na asilimia 40 hubaki kwenye mapato ya Halmashauri husika kwa ajili ya shughuli za uhifadhi wanyamapori na
mazingira yake. kuhusu michango ya makampuni kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijiji alitanabiasha kuwa sheria ya wanyamapori
na.5 ya mwaka 2009 inatambua uhifadhi wa wanyamapori kwa njia ya matumizi endelevu hivyo inaainisha kila kampuni yenye kupewa kitalu
kwenye eneo husika inatakiwa kuchangia Dola 5000 za kimarekani kwa ajili ya shughuli za amendeleo kwenye vijiji na fedha hizo zinagawanywa
kulingana na idadi ya vijiji vinavyozunguka hifadhi husika, hivyo ni takwa la kisheria na siyo hiari kuchangia fedha hizo kila mwaka ama
msimu wa uwindaji unapoanza. misaada mingine nje ya hapo hutolewa na makampuni husika kwa hiari ili kuboresha mahusianao.
Makampuni hayo ni pamoja na Robin Hurt Safaris, Mwatisi Hunting Safari, Old Nyika Safari and Royal Holdings Safaris na Northen Safari enterprises. ambapo vijiji vilivyopata
mgao huo ni pamoja na Kambikatoto, Bitimanyanga, Mafyeko, Lualaje na Mtanila.
katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wawakilishi wa makampuni ya uwindaji kitalii, wataalam wa misitu na wanyamapori pamoja na wadau mbalimbali;
Watendaji wa vijiji vinavyopitiwa na hifadhi walipata fursa ya kutoa mchanganuo wa Mapato na matumizi ya fedha kulingana na mgao wa makampuni ya uwindaji katika vijiji vyao.
Kaimu Mkurugenzi Bw.Weston Njeje aliyesimama, Mkuu wa wiaya ya Chunya Bi.Rehema Madusa(kulia kwake), Kaimu Afisa Maliasili Bw.Lucas Theodory (kushoto), na Afisa Maliasili Mkoa (kulia)
Wawakilishi wa Makampuni ya Uwindishaji kitalii
Afisa Wanyamapori Chunya Ndg.Jacob Mpinga (aliyesimama) akichangia mada, kulia kwake ni mwakilishi wa WCS na kushoto kwake ni Bi Simphorose Kavishe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.