Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga amekabidhi vikundi vya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hundi yenye thamani ya shilingi million 789,500,000 kwaajili ya kuwezesha makundi hayo kujikwamua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na hatimae kuinua pato la taifa.
Mhe Batenga amekabidhi hundi ya millioni 789,500,000 tarehe 21/11/2025 kwa vikundi 82 ambapo wanawake ni 40, vijana 39 na watu wenye ulemavu 3 katika ukumbi wa Sapanjo Halamashauri ya Wilaya ya Chunya.
Aidha Mhe. Batenga amesema kuwa mkopo wa asilimia 10 ni mpango wa serikali kuwawezesha wananchi wake kiuchumi lakini pia kuwawezesha waweze kujiajiri na kuajiri wengine ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na maisha bora na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
“Mikopo ya asilimia kumi ni mpango wa serikali kuwasaidia wananchi kujiwezesha kiuchumi ili kila mmoja aweze kusaidia familia yake ,lakini pia kumsaidia mwananchi kuwa na kazi halali inayoweza kumuingizia kipato kwaajili ya familia na kuwezasha kuwa na uchumi jumuishi ambapo kila mwananchi anauwezo wa kujipatia kipato” alisema Mhe.Batenga.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi hundi Katibu wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya ndugu Charles Jokery ametoa msisitizo juu ya kulinda amani kwani pasipo kuwa na amani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana hivyo maendeleo ya watu yanatokana na kuwepo kwa amani katika Taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona amewahakikishia wananchi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya itaendelea kuhakikisha inatenga fedha kwaajili ya mkopo wa asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake , vijana na watu wenye ulemavu kari makusanyo yatakavyokuwa yanaongezeka sambamba na kuendelea kujenga miradi ya maendeleo kupitia mapato ya Halmashauri.
Akisoma taarifa ya Vikundi ndugu Antony Ndenga amesema kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba kwa mwaka wa fedha 2025/2026 jumla ya vikundi 82 ndivyo vilivyo kidhi vigezo vya kupata mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri kupitia mapato ake ya ndanii kwaajili ya kwenda kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Wakizungumza kwa niabaya wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 Daud Kachambuka,Neema Jeremiah wameishukuru serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wake kwa kuwawezesha kiuchumi kupitia mkopo unaotolewa na Halmashauri bila riba yoyote.
Mikopo ya asilimia 10 hutolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa awamu tofauti tofauti ili kuwezesha vikundi vya wanawake ,Vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni adhima ya serikali kuwawezesha wananchi wake kiuchumi .

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akizungumza adhima ya serikali ya kutoa mkopo wa asilimia 10 wakati wa hafla ya kukabidhi hundi vikundi 82 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu katika ukumbi wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya

Vikundi vya Wanawak,vijana na watu wenye ulemavu vikipokea hundi yenye thamani ya shilingi millioni 789,500,000 kwaajili ya fanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujipatia kipato.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wialaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona akiwahakikishia wananchi kwendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa kadri makusanyo yanavyoongezeka ili kwawafikia watu wengi zaidi .

Vikundi vya Wanawake Vijana na watu wenyeulemavu wakifuatilia hotuba wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi ya mkopo wa asilimia kumi unaotolewa na Halmashauri .
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.