• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

WAJUMBE WA BARAZA LA BIASHARA CHUNYA WAMETOA YA MAYONI

Imewekwa: November 20th, 2025

Baraza la biashara Halmashauri ya wilaya ya Chunya limepania kuwafikia wafanyabiashara wote wa wilaya ya Chunya bila kujali biashara wanayofanya na eneo wanalopatikana huku lengo likiwa kurahisisha uendeshaji wa biashara kwa wananchi wa Chunya na kufikia azma ya kujiletea maendeleo binafsi na hatimaye maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wajumbe wa baraza la biashara katika kikao kilichoketi 19.11.2025 katika ukumbi wa Mwanginde Hall uliopo jengo jipya la utawala la Halmashauri ya wilaya ya Chunya wajumbe wakiongozwa na Mwakilishi wa katibu mtendaji TNBC wajumbe wameeleza nia ya Serikali ya uundwaji wa Mabaraza ya Biashara nchini

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara Taifa (TNBC) ndugu Patrick Mavika amesema lengo la Serikali ni kuona Mabaraza yote ya Biashara yanakuwa hai na yanaleta msaada kwa wafanyabiashara na Serikali huku akiwakumbusha wajumbe kupendekeza njia sahihi ya kushughulikia changamoto mbalimbali wanapoziwasilisha.

“Ndugu wajumbe kikao hiki sio cha kawaida maana leo tumekuja tuweze kujengeana uwezo ili mabaraza yetu yawe mabaraza yawe yenye tija. Mfanyabiashara asije hapa kupoteza muda” Alisema Patrick Mavika Mwakilishi wa Katibu mtendaji Baraza la Biashara (TNBC)

Wajumbe wa baraza hilo kwa nyakati tofauti katika kikao hicho nao wametoa maoni yao ili wafanyabiashara wa Chunya wafanye biashara katika mazingira mazuri na yenye tija kwao na hatimaye kuleta hamasa ya ulipaji wa kodi mbalimbali kwa mujibu wa Sheria.

“Kama Sehemu ya wafanyabiashara wanaoenda minadi naomba tutazamwe vizuri eneo la mikopo kwa wafanyabiashara wanaoenda minadi, tupatie elimu ya fedha maana wako watu wanapata fedha nyingi lakini hawana elimu ya fedha pia tupatiwe elimu ya mikopo kwani wafanyabiashara wengi kwakukosa elimu wamejikuta wakiangukia kwenye mikopo umiza kutokana na kukosa Elimu hivyo kupitia baraza hili tutazamwe kwa jicho pevu” Alisema ndugu Abisai Ngao, Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Minadani wilaya ya Chunya na Mkoa wa Mbeya

“Mimi nilikuwa na maombi kuhusu hili baraza letu la wafanyabiashara, kwanza tunatakiwa tujue umuhimu wa sisi kuhudhuria baraza hili, mfanyabiashara mwingine hawezi kuelewa maana ya baraza hili, sisi tunaohudhuria ni kwasababu tunajua umuhimu wake ingawa ni vigumu hata kwangu kuhudhulia ikiwa sioni umuhimu wake, Hivyo naomba tuongeze wigo wa wadau wa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na wamachinga ili baraza lisionekane linalenga wafanyabiashara wakubwa tu” Amesema Peter Mayala, Mwenyekiti wa wafanyabiashara za Mazao wilaya ya Chunya.

“Kwa namna ya pekee naomba nishukuru uongozi wa Baraza la biashara la wilaya ya Chunya kwakuhakikisha wajumbe wanafika katika kikao hiki lakini pia nipongeze mahudhurio mazuri ya wajumbe kutoka pande zote mbili, Mahudhurio haya yameonesha utofauti katika wilaya ya nne tulizofika, Hongereni Chunya”

“Pia wafanyabiashara eneo tunaloweza kufanya kimbilio letu ni baraza la wafanyabiashara hebu tuungane kulitumia baraza let una palepoonekana kuleta shida tuungane tuwaombe wahusika kikao a zungumze” aliendelea kusisitiza Erick Sichinga Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya

Mwenyekiti wa TCCIA wilaya ya Chunya Ndugu Hassan Kapunga aliwataka wafanyabiashara kutumia Baraza hilo vizuri ikiwa ni pamoja na kuleta malalamika, mapendekezo pamoja na maoni mbalimbali yanayoweza kuleta mazingira rafika ya biashara wanazofanya.

“Tuna vyombo hivi ili kurahisisha mijadala ya wanaoonewa na wanao onea na kufikia suluhu ya changamoto zetu nah ii ndo sababu kubwa ya kuwa na vyombo hivi, wafanyabiashara Baraza hili ni let una Chunya pia ni yetu hebu tuchangamke” Amesema Ndugu Hassan Kapunga Mwenyekiti TCCIA wilaya ya Chunya

Kikao cha Baraza la Biashara Chunya kimeketi tarehe 19.11.2025 kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wapya walioteuliwa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa faida yaw engine wengi wanaowawakilisha kulingana na biashara wanazofanya


Taarifa hii inapatikana Toutube kwa kubonyeza kiunganishi hapa chini

https://www.youtube.com/watch?v=-gAljjNCjj4&t=449s

Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji TNBC Ndugu Patrick Mavika akizungumza wakati wa Baraza la Biashara Chunya

Afisa Biashara wilaya ya Chunya Ndugu Lodrick Mwakisole akizungumza jambpo wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyabiashara kilichoketi ukumbi wa Mwanginde Hall

Matangazo

  • KUPIGA KURA YA RAIS KITUO AMBACHO HAUKUJIANDIKISHA September 15, 2025
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • MHE MASACHE AUNGANA NA VIONGOZI WA DINI NA SERIKALI KUSISITIZA UWEPO WA AMANI.

    December 04, 2025
  • WATALAM NA MADIWANI WAASWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI.

    December 02, 2025
  • CHUNYA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO VVU

    December 01, 2025
  • HAKIKISHENI MASHAMBA YOTE YA SHULE YANALIMWA MSIMU HUU WA MVUA.

    November 27, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.