Katibu tawala Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero amewataka watendaji kata kwa kushirikiana na Maafisa elimu kata, walimu wakuu na wakuu wa Shule kuhakikisha mashamba ya shule yanalimwa kwa msimu huu wa mvua ulioanza ili kuharahisisha upatikanaji wa chakula Shuleni ikiwa ni matakwa ya serikali ya kuhakikisha watoto wote wanapata chakula Shuleni.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 27/11/2025 wakati wa kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe ngazi ya kata kwa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichoketi katika Ukumbi wa mikutano wa Mwanginde hall Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Tumeanza msimu wa kilimo hakikisheni kila Shule msimu huu wa mvua inalima kwaajili ya Chakula Shuleni ,lakini pia nunueni mbegu za ruzuku zinazotolewa na serikali kwaajili ya kupanda katika mashamba hayo na mjitahidi kupanda kwa wakati ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa “ amesema Anakleth
Aidha katibu tawala ametoa msisitizokatika msimu huu wa mvua kuhakikisha tahadhali zinachukuliwa ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na magonjwa mengine yanayoweza kutokea hususani katika kipindi hiki cha mvua.
Akizungumza katika kikao hicho Mganga mkuu Wilaya ya Chunya Dkt Zuberi Mzige amesema kuwa mapambano dhidi ya utapiamlo yanapaswa kuanzia ngazi ya familia huku akitoa rai kwa waratibu wa lishe kuhakikisha wanalishughulikia jambo hilo katika maeneo yao ili kutoa msaada pindi inapotokea kuna mtu kapata changamoto hiyo ili kuhakikisha anapata matibabau na kurejea katika hali yake.
Afisa Lishe wa Wilaya ya Chunya ndugu Erick Kessy akisoma taarifa ya utekelezaji ngazi ya kata robo ya kwanza ya july hadi Septemba kwa mwaka 2025/2026 kadi alama ni kiashiria kinachoonyesha namna ambavyo ngazi ya kata imetekeleza majukum yake ya kuwafikia wananchi ikiwa ni pamoja na kuibua watoto wenye changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na utapiamlo.
Naye afisa lishe Wilaya ya Chunya ndugu Saimoni Mayala amepongeza juhudi za watendaji na waratibu wa lishe kwa kupambana kuhakikisha chakula kinapatikana Shuleni na watoto wanapata chakula shuleni lakini pia ameendelea kusisitiza ushirikiano baina ya watendajina walimu wakuu na wakuu wa Shule kwani walimu peke yao hawawezi kutimiza adhima ya upatikanaji wa chakula Shuleni.
Kikao cha tathimini mkataba wa lishe ngazi ya kata hufanyika kila robo ili kuona hali ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kubaini mafanikio na changamoto zilizojitokeza na kuangalia namna ya kukabiliana nazo.

Katibu tawala Wilaya ya Chunya akitoa maelekezo ya kuhakikisha mashamba ya Shule yanalimwa wakati wa kikao cha tathimini ya makataba wa lishe ngazi ya kato robo ya kwanza kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwanginde hall Halmashauri y Wilaya ya Chunya.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dkt Zuberi Mzige akitwakumbusha kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipiko kwa kipindi hiki cha mvua wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha tathimini ya mkataba wa lishe ngazi ya kata.

Afisa lishe ndugu Saimon Mayala akifafanua jambo wakati wa kikao cha tathimini ya Mkataba wa lishengazi ya kata katika ukumbi wa mikutano wa Mwanginde hall.

Watendaji wa kata, waratibu wa lishe na waratibu elimu kata wakifuatilia agenda mbalimbali wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha tathimini ya Mkataba wa lishe ngazi ya kata.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.