Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Lupa wakili Athumani Bamba amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo kuwa na lugha nzuri kwa wateja wao ambao ni wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuwachukulia madhaifu yao lakini pia , kuwaelekeza lugha nzuri pasipo kutumia matusi au maneno yasio faa kwa wapiga kura.
Kauli hiyo ameisema leo tarehe 27/10/2025 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo yaliyofanyika katika ukumbi wa Omary City Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Tukawe na lugha nzuri kwa wateja wetu ambao ni wapiga kura sisi hapa ni watumishi wa tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na wapiga kura ndio wateja wetu,kwahiyo tunapaswa kuwa vizuri kwa wateja mtu anaweza kuja na chngamoto zake lakini wewe mueleweshe mtu aelewe ili waweze kupiga kura sawa sawa na kutoka pasipo kuwa natatizo lolote” amesema Wakili Bamba
Aidha Wakili Bamba ameendele kuwakumbusha wasimamizi wa na wasimamizi wasaidizi wa vituo kuyafanyia kazi na kuyazingatia yale yote waliyoelekwezwa tangu walipoanza mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kulindana kuthamini kiapo walichaapa na kutojihusisha na mambo ya Vyama ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi .
Naye Afisa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Ridhiwani Mshigati amewakumbusha wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo kutokufanya yale yote ambayo hawapaswi kuyafanya ikiwa ni pamoja na matumizi ya simu, lugha za matusi , kuchelewa kufika katika kituo ambacho msimamizi amepangiwa na mambo mengine mengi na kuvaa mavazi yenye staha.
Wakizungumza kwa niaba ya wasimamizi wengine Maria Mwanijembe , Alex John wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kufanya kazi yao kwa ufasaha na kuhakikisha zoezi la upigaji kura linafanyika kwa kuzingatia maelekezo ya tume kama ambavyo wamefundishwa.
Mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo yamedumu kwa muda wa siku mbili tarehe 26 na 27 Octoba 2025 ambapo mambo mbalimbali yamefundishwa ikiwa ni pamoja na namna ya kujaza fomu mbalimbali za Uchaguzi pamoja , kujaza mikataba na mbambo mengine mengi kwaajili ya uchaguzi mkuu tarehe 29 Oktoba 2025
.

Maimamizi wa uchaguzi jimbo la Lupa wakili Athuman Bamba akitoa msisitizo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi ngazi ya vituo wakati wa kufunga mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi katika Ukumbi wa omary city.

Afisa uchguzi halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Ridhiwani Mshigati akiwakumbusha wasimamizi na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya vituo kutokufanya yale yote ambayo hawapaswi kufanya katika vituo.

wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo wakiendelea kufuatilia maelekezo yanayotolewa na wakufunzi katika ukumbi wa Omary City Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.