Shughuli za kibinadamu zikiwemo uchimbaji madini na kilimo ni chanzo cha uharibifu wa mazingira Wilayani Chunya.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wikaya ya Chunya, Mayeka S. Mayeka alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani inayofanyika Juni 5 ya kila mwaka.
“Kwa upande wetu Chunya tuna shughuli kuu mbili za kiuchumi, uchimbaji wa madini na kilimo cha tumbaku, shughuli hizi mbili ndizo zinazoongoza kwa ukataji miti kwa kiasi kikubwa,” alisema Mayeka.
Aidha, Mayeka ameainisha vitendo vya uchomaji moto mashamba na misitu kuchangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi na uharibifu wa mazingira Mkoani Mbeya.
“Katika mkoa wetu tuna changamoto ya moto, hiki ni kikwazo kikubwa katika jitidaha zetu za kuhifadhi mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji na misitu, shughuli za uwindaji hasa Wilaya za Chunya, Mbalali na Mbeya vijijini, aidha shughuli ya uchimbaji wa madini ni kinara kwa uchomaji wa moto pindi wanapotafuta maeneo yenye dhahabu.” Alisema Mayeka.
Kadhalika Mayeka amesema hali ya mazingira kidunia na kitaifa si nzuri sana ambapo bado kazi kubwa inahitajika kufanyika katika harakati za utunzaji wa mazingira, ikiwemo Mkoa wa Mbeya kuhakikisha mazingira yanakuwa endelevu ili vizazi vingine vikute mazingira yaliyo salama.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mbeya Ndg. Said Madito ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanatunza mazingira kwa ajili ya wao na vizazi vijavyo.
“Sisi kama mkoa tutahakikisha tunashirikiana na wadau wote kwa ajili ya kuyatunza mazingira ili kusudi zoezi la kilimo, uchimbaji wa madini, ufugaji ziendane na uhifahi wa mazingira.” Alisema Madito.
Madito aliongeza kwa kusema kuwa, kaulimbiu ya mwaka huu inakumbusha mambo matatu yakiwemo kupanda kwa joto duniani, wajibu wa kutunza viumbe hai na jambo la tatu ni suala la uchafuzi wa mazingira.
“Sisi kama Mkoa ni sehemu ya jamii ambayo inatakiwa istaarabike kwa kuyatunza mazingira, hivyo tuepuke uchafuzi wa mazingira,” amesema Madito.
Kaulimbiu ya kitaifa ya siku ya uhifadhi wa mazingira duniani ilisema, “Tanzania ni moja tu, tunza mazingira”
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka akipanda Mti katika eneo la Shule ya Msingi Makongolosi ikiwa ni katika Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Wanakikundi cha TOFAA wakionyesha bango lenye ujembe usemao " Miti ni sehemu ya maisha yetu kila mmoja anawajibu wa kuitunza" kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya Mhe. Noel Chiwanga akipanda mti eneo la shule ya Msingi Makongolosi ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Dunini
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.