Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga amemwambia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kuwa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Wilaya ya Chunya unakwenda vizuri huku akitaja baadhi ya maeneo kama ujenzi na usimaz mzuri wa miradi ya maendeleo , ukusanyaji wa mapato ya Serikali pamoja na kutatua kero mbalimbali zzinazowakabili wananchi.
Kauli hiyo ameitoa April 6, 2024 wakati akitoa salamu za Serikali mbele ya Mwenyekiti wa Chacha Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa wazazi wa jumuiya ya Chama cha Mapinduzi yaliyoadhimishwa kimkoa katika kata ya Sangambi, Halmashauri ya wilaya ya Chunya.
“Nikuhakikishie utekelezaji wa Ilani ya chama kwa Wilaya ya Chunya tuzo vizuri sana hapa walikuwa wanazungumza juu ya kituo cha afya cha Sangambi naomba nikuhakikishie kwamba kituo hiki tunakijenga kwa kutumia mapato ya ndani lakini pia kwa upande wa ukusanyaji wa mapato ya serikali kwasasa hivi Wilaya ya Chunya ndio tunaongoza kwa ukusanyaji wa mapoato kwa Mkoa wa Mbeya hii ni kutokana na jinsi ambavyo tumejipanga kuitekeleza Ilani” alisema Mhe.Batenga
Akizungumza na hadhara iliyokusanyika katika shrehe hizo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ndugu Patrick Mwalunenge aliyekuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ameitaka jamii kuwalea watoto katika maadili mazuri ili wawe waadilifu katika maisha yao ya baadaye huku akionya malezi mabaya yanayotolewa na wazazi na walezi kwa watoto wao.
“Leo niwaambie wanasangambi tatizo la mmomonyoko wa maadili ni kubwa sana tumeona kila siku Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan akitumia gharama kubwa sana kuwabadilisha vviongozi katika nafasi zao kutokana na ubadhilifu na udanganyifu katika mali za umma hayo yote yanatoka kwetu sisi kutokana na malezi kwasababu wale ni watoto ambao tumewalea sisi wenyenyewe”. Alisema Mwalunenge.
Naye Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ndugu Jmames Mwampondele amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo kama jumuiya ya wazazi ni kuhakikisha wanasimamia maadili, malezi , Mazingira pamoja na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukatili wa Kijinsia kwa kutoa elimu kwa wanajamii na wana CCM ili kutengeneza jamii bora.
Maadhimisho hayo yameadhimishwa Aprili 6, yakiongozwa na na kauli mbiu isemayo Ushindi wa CCM 2024-2025 Umoja wa Wazazi Tupo mstari wa Mbele yameenda sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali kuhusu mmomonyoko wa maadili kutoka kwa wadau na taasisi mbalimbali, na yamehudhuriwa na viongozi wa chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Mkoa hadi ngazi ya jijiji, wanachama wa Chama cha Mapinduzi pamoja na viongozi wa Serikali kutoka ngazi Mbalimbali za uongozi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ndugu Patrick Mwalunenge mgeni rasmi akizungumza mambo mbalimbali ya juu ya utekelezaji wa ilani pamoja na masuala ya mmomonyoko wa maadili katika jamii wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa wazazi Jumuiya CCM yaliyoadhimishwa katika kata ya Sangambi Wilayani Chunya.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Wananchi waliojitokeza katika sherehe za kilele cha wiki ya Maadhimisho ya Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Chunya kata ya Sangamgi
Mgeni rasmi ndugu Patrick Mwalunenge Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya akiserebuka pamoja bandi ya Yangagilashila wakati wa sherehe za kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM yaliyofanyika katika kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.