Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kusimamia zoezi la usafi wa mazingira kwa wananchi wa wilaya hiyo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza ikiwemo kipundupindu.
Mhe. Batenga ametoa agizo hilo, Septemba 20, 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya usafishaji duniani wakati akihutubia mkutano wa wananchi soko la Uhindini Kata ya Chokaa Wilayani Chunya ambapo amesisitiza matumizi bora ya choo, kunawa maji tiririka na sabuni kunapunguza athari za kupata ugonjwa wa kipindupindu kwa asilimia 40 huku akimtaka Afisa Afya wa Wilaya kuhakikisha wanawatoza faini wote wanaokiuka.
“Mkurugenzi hakikisha kila mtu anafanya usafi kwenye eneo lake utaniambia wangapi hawajafanya usafi, faini itasaidia kurebisha tabia za uchafu” amesema Mhe. Batenga.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Chunya amewakumbusha wananchi wa Wilaya hiyo, hivi karibuni wilaya hii ilikumbwa na mlipuko wa kipindupindu Chunya iripoti wagonjwa ishirini na tano (25) ambapo sababu kubwa ni uchafu wa mazingira.
“Kulikuwa na kipindupindu Wilaya ya Chunya, hii imetokana uchafuzi wa mazingira, kutozingatia kanuni bora za mlo na matumizi mabaya ya Choo, kila mwananchi afanye usafi kwenye eneo lake pamoja na kufyeka maeneo yanayozunguka nyumba zenu” amesema Mhe. Batenga.
Wafanyabiashara wa Soko la Uhindini wilayani Chunya walimueleza Mhe. Batenga changamoto zilizopo kwenye eneo hilo ikiwemo ukosefu wa maji safi, ubovu wa miundombinu na ukosefu wa dampo kwaajili ya kutupa taka ambapo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, wakili Athumani Bamba amewahikishia wafanyabiashara hao kuwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kero zote walizozieleza zitafanyiwa kazi.
Wilaya ya Chunya imeadhimisha siku ya usafishaji duniani kwa kufanya usafi maeneo ya soko la Uhindini pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo hayo kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko, kauli mbiu ya usafishaji duniani mwaka 2024 ni “Uhai hauna mbadala, zingatia usafi”.
Kaimu Afisa Mazingira Ndugu Baraka Kipesha akisoma Taarifa ya Mazingira Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya mapema leo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Usafishaji Duniani ambapo kiwilaya yamefanyika kwa kufanya usafi soko la Uhindini na baadaye Mkuu wa wilaya kuzungumza na wananchi waliojitokeza
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga akizungumza na wananchi waliojitokeza kuadhimisha siku ya usafishaji Duniani ambapo kwa wilaya ya Chunya maadhimisho hayo yamefanyika Soko la Uhindini lililopo Kata ya Chokaa
Mkuu wa wilaya ya Chunya akitoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali wa kata ya Chokaa, viongozi wa Halmashauri pamoja na viongozi wa Soko kuzingatia usafi wakati wa maadhimisho ya siku ya usafishaji
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.