Afisa afya na mazingira kutoka wizara ya afya Ndugu Ramadhani Bofu amemtaka Afisa Afya wa Hospital ya Wilaya kuhakikisa anawajengea uwezo wataalam mbalimbali wanaohusika na usafi wa mazingira hospitali ya wilaya chunya ili kuhakikisha mazingira ya Hospital yanakuwa safi na salama kila wakati
Maagizo hayo aliyatoa jana julai 10,2023 wakati alipokagua zoezi la usafi wa mazingira ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Mashindano ya usafi wa mazingira yanayofanyika kila mwaka ili kuhamasisha nakuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama ili kuwasaidia wananchi kujikinga na kujiepushana maradhi mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu wa mazingira.
‘’Hakisha unajiwekea utaratibu wa kuwajengea uwezo wataalamu mbalimbali wanaohusika na usafi wa mazingira angalau kila baadaya miezi mitatu (3) ikiwa ni pamoja na kutembelea vifaa vya kuhifadhia taka mara kwa mara kuona kama zinahifadhiwa kwa usahihi na zinateketezwa katika eneo maalumu lililotengwa kulingana na aina ya taka hizo na kuhakikisha kila aina ya taka inawekwa katika chombo husika cha kuhifadhia taka hizo nazile za kutupwa katika shimo la taka zitupwe katika shimo
Awali akitoa taarifa fupi ya usafi wa Mazingira afisa afya wa kata ya itewe Ndugu Moses Katamba amesema kuwa usafi wa mazingira ni Agenda ya kudumu na wamekuwa wakihamasisha wananchi kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila jumamosi lakini pia wameendelea kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora na kuhakikisha kila kaya inakuwa na ndoo yenye maji safi kwaajili ya kunawa mikono mtu anapotoka chooni, shimo la taka pamoja na vichanja.
‘’Tumejiwekea sheria ndogondogo ikiwemo faini ya Tsh 5000 hadi Tsh 50,000 ambazo hutozwa watu wanaokaidi kufuata maagizo ya kuweka mazingira yao katika hali ya usafi na salama na wakati mwingine tumekuwa tukiwafikisha mahakamani, lengo ni kuweka mazingira safi na salama kwa afya zetu lakini pia kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababishwa na uchafu wa mazigira’’
Katika nafasi nyingine Ndugu Ramadhani Bofu ametoa ushauri kwa uongozi wa shule ya msingi Chunya kati kuhakikisha wanakuwa na mpango endelevu wa kuhakisha mazingira yanakuwa katika hali ya ubora kwa kutenga bajeti itakayokuwa inawasaidia kutatua changamoto ndogondogo na kuacha kusubiri mpaka fedha za mfadhili amewataka pia kuhakikisha wanaeka milango katika kila chookwa vyoo vichache ambovyo vinatumia mlangommoja ili kuzingatia usiri wa mwanafunzi anapokuwa chooni.
‘’Ni vuzuri kuwa na mpango endelevu wa kuhakikisha mazingira na miundombinu inakuwa katika hali ya ubora wakati wote kwa kutenga bajeti itakayo kuwa inawasaidia kutatua changomoto ndogondogo za miundombinu inapokuwa imeharibika kwa wakati na kuacha kusubiria mpaka fedha za mafadhili ‘’
Firdaws Hamidu mwanafunzi wa darasa la sita (vi B) shule ya msingi Chunya kati ni miongoni mwanafunzi waliopo katika klabu ya usafi wa mazingira mashuleni ( school water Sanitation and hygiene club) ameeleza mambo mbalimbali wanayojifunza kwenye klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wanafunzi wenzao kuzingatia usafi wao binafsi wanapokuwa shuleni na majumbani kwa kuweka safi mazingira yanayowazunguka na kunawa mikono mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Zezi la ukaguzi wa usafi wa mazingira limefanyika katika maeneo mbalimbali ya hospitali ya wilaya ikiwemo maeneo yakuhifadhia taka,mitambo mbalimbali, mindombinu ya maji, vyoo na maeneo yote kwa ujumla ,zoezi hilo liliendelea pia katika kata ya Itewe ambapo ilifanyika katika vijiji viwili (2) ambovyo ni Chunya Mjini na Sinjilili katika kaya mbalimbali, makanisa, na mahakamaya mwanzo. Zoezi hilo lilihusisha wataalam mbalimbali akiwemo kaimu afisa afya na Mazingira kutoka Mkoani Ndugu David Mwakasege ,Afisa afya wa wilaya Ndugu Baraka Kipesha,afisa afya kata itewe Moses katamba na maafisa mbalimbali katika ngazi za vijiji.
Afisa afya na mazingira ndugu Ramadhani Bofu (alievaa shati la kitenge) kutoka wizara ya afya akikagua shimo la taka la hospitali ya wilaya ya chunya
Afisa afya na mazingira kutoka wizara ya Afya akitoa maelekezo ya kurekebisha bomba la maji kwa afisa afyaa wa wilaya ndugu Baraka Kapesha
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.