Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya umefikia kiwango wa lenta ambapo ni karibu asilimia 40 ya ujenzi na fedha zilizotumika mpaka Sasa ni zaidi ya milioni 40 kati ya milioni 150 zilizotolewa na serikali kuu kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo. Lengo la serikali ni kuhakikisha watumishi wanapata makazi mazuri ili waweze kuwatumikia wananchi wa Tanzania bila Changamoto yoyote
Chini ya usimamizi wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmsahauri ya wilaya ya Chunya Ndugu. Tamim Kambona na Wahandisi wa ujenzi wilaya ya Chunya pamoja na kuendelea kusimamia miradi mbalimbali inayojenga wilayani Chunya wanasimamia ujenzi wa Nyumba hii kwa ukaribu ili kuhakikisha thamani ya fedha iliyotolewa inafanana na ubora wa mradi husika.
Muonekano wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji Inayoendelea Kujengwa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.